Home » » MKOA WA SHINYANGA WATOA ZAIDI YA MILIONI 41KUSAIDIA WAATHIRIKA WA TETEMEKO KAGERA.

MKOA WA SHINYANGA WATOA ZAIDI YA MILIONI 41KUSAIDIA WAATHIRIKA WA TETEMEKO KAGERA.


 Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi. Zainabu Telack (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Kijuu (kulia) baadhi ya misaada iliyotolewa na wananchi wa mkoa wa Shinyanga kwa waathirika wa tetemeko la ardhi Kagera.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Kijuu akitoa shukrani baada ya kupokea misaada kutoka mkoa wa Shinyanga



Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi. Zainabu Telack (kulia) akitoa maelezo kuhusu msaada wa vifaa vya ujenzi na chakula kutoka kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga. Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bw. Albert Msovela.

 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Kijuu (wa nne kushoto) na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi. Zainabu Telack (wa pili kulia) wakielekea eneo la kupokea misaada iliyotolewa na wananchi wa Shinyanga.



(Picha/Habari na Eleuteri Mangi, Bukoba)
Mkoa wa Shinyanga umekabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi na chakula vyenye thamani ya Sh. milioni 41,172 kwa uongozi wa mkoa wa Kagera ili kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea mkaoani humo hivi karibuni.


Makabidhiano hayo yalifanywa leo mjini Bukoba kati ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi. Zainabu Telack ambaye aliambatana na baadhi ya viongozi wa mkoa na viongozi wa dini ambapo mkoa wa Kagera umewakilishwa na Mkuu wa Mkoa wa huo Meja Jenerali Mstaafu Salim Kijuu.


Wananchi wa mkoa wa Shinyanga wameguswa na kadhia iliyopata wananchi wa Kagera, hivyo tukaamua kukusanya nguvu ya pamoja kama mkoa ili kuwafariji Watanzania wenzetu kutokana na matatizo waliyoyapata” alisema Bi Zainabu.

Mkuu huyo wa mkoa alifafanua mchango wa misaada waliyotoa kuwa ni paamoja na mabati ya geji 28 1400, saruji mifuko 750, mchele kilo 600, mahindi kilo 100 paamoja na nguo.

Bi. Zainabu aliongeza kuwa michango ya msaada huo imeunganishwa nguvu kutoka Serikali ya mkoa wa Shinyanga, taasisi za Serikali na zisizo za kiserikali, sekta binafsi, masshirika ya dini, asasi za kiraia, wafanyabiashara, mogodi ya madini iliyopo mkoani humo na wadau wengine wa maendeleo.

Akitoa shukrani mara baada ya kupokea msaaada huo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Kijuu  amewashukuru wananchi wa Shinyanga kwa kuwafariji, majitoleo yao kwana kuwajali katika kipindi hiki cha mpito cha athari za tetemeko lililoukumba  mkoa huo.


 


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa