RC MACHA AZINDUA BANGO LA KISWAHILI MRADI UJENZI BARABARA YA LAMI KAHAMA –BULYANHULU JCT- KAKOLA, AIPONGEZA TANROADS

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha (aliyevaa miwani)akizindua Bango la Kwanza lililoandikwa kwa Lugha ya Kiswahili linaloelezea utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa barabara ya Kahama – Bulyanhulu JCT- Kakola 

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amezindua Bango la Kwanza lililoandikwa kwa lugha ya Kiswahili linaloelezea utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa barabara ya Kahama – Bulyanhulu JCT- Kakola  yenye urefu wa Km 73 ikiwa ni utekelezaji wa ushauri wake wa kuanza kutumia Lugha ya Kiswahili  katika Mabango  yote ya miradi ndani ya Mkoa wa Shinyanga.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo Jumatatu Septemba 23,2024 Mhe. Macha amesema Lugha ya Kiswahili inatumiwa na wananchi wengi na  kwa kuwa miradi yote ni ya wananchi hivyo wanapaswa kuelewa nini kimeandikwa na nini kinatekelezwa na Serikali katika maeneo yao.

“Nawapongeza TANROADS kutayarisha na kuweka bango hili kwenye mradi wa ujenzi wa Kilometa 73 ya Kahama hadi Kakola kwa kiwango cha Lami ukaogharimu zaidi ya shilingi Bilioni 101 .2. Hili ni bango la Kwanza  kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili katika Mkoa wa Shinyanga. Naagiza pia kwenye maeneo mengine miradi sekta mbalimbali mabango yaandikwe kwa Lugha ya Kiswahili, hata kama mtaweka Bango la Kiingereza lakini pia muweke la Kiswahili kwani Lugha ya Kiswahili inajitosheleza kwa kila kitu”,ameeleza Mhe. Anamringi.

"Nawapongeza sana Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Shinyanga chini ya Mhandisi Samwel Joel Mwambungu kwa kuwa wa kwanza kutekeleza ushauri wangu wa kuanza kutumia Lugha ya Kiswahili katika mabango yote yanayoelezea miradi inayotekelezwa kwa wananchi ndani ya Mkoa wa Shinyanga, hongera sana Meneja Mhandisi Mwambungu," amesema Mhe. Macha.

BENKI YA CRDB YATUMIA MAADHIMISHO YA SIKU YA USHIRIKA DUNIANI 'SUD' KUONESHA FURSA ZA UWEKEZAJI


Benki ya CRDB imeshiriki maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani (SUD) duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Tabora katika Viwanja vya Ipuli.

Maadhimisho hayo yaliyoanza tarehe 29 Juni 2024 na kuhitimishwa leo tarehe 6 Julai,2024 yalifunguliwa na Naibu Waziri wa Kilimo Mh. David Silinde na kufungwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko.

Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Abdulmajid Nsekela aliungana na wafanyakazi wa Benki ya CRDB kutoka Makao Makuu wakiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Kilimo Biashara, Maregesi Shaaban, pamoja na wafanyakazi wa Kanda ya Magharibi wakiongozwa na Meneja wa Kanda hiyo, Jumanne Wagana.

Benki ya CRDB ikiwa ni mdau mkubwa wa sekta ya ushirika nchini, Benki ambayo pia ndio mdhamini mkuu  imetumia maadhimisho hayo kuonesha fursa za uwezeshaji zinazotolewa kwa wateja wake waliopo kwenye mnyororo wa thamani katika sekta za kilimo, uvuvi, ufugaji, viwanda na usafirishaji.

#CRDBBank
#UlipoTupo


SHEREHE YA WENYE VITI WA MITAA ,VIJIJI NA VITONGOJI MANISPAA YA SHINYANGA YAFANA SHY COM

Wenyeviti wa mitaa ,vijiji na vitongoji Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wamefanya sherehe ya kujipongeza kwa utendaji kazi wao wa miaka mitano.
Sherehe hiyo imefanyika katika ukumbi wa chuo cha walimu Shinyanga ikiambatana na zoezi la kuchangia damu katika benki ya damu iliyopo katika hospitali ya Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga kwa lengo la kusaidia makundi ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu wakiwemo wajawazito,watoto na waathirika wa ajali.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika Sherehe hiyo Anord Makombe ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga Mjini amewataka wenyeviti hao kuendelea kufanya kazi kwa bidii ya kuwahudumia wananchi katika kipindi hiki ambacho wanajiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa.
Naye mwenyekiti wa Mtaa wa Miti Mirefu Moke warioba ambaye pia ni mwenyekiti wa wenyeviti wa serikali za mtaa Manispaa ya Shinyanga amewashukuru wenyeviti kwa ushirikiano wao ambao wanaendelea kumpatia na kuomba ushirikiano huo uendelee wakati wanapoendelea kuwatumikia na kutatua kero za wananchi.



















MAADHIMISHO YA UPANDAJI MITI KITAIFA SHINYANGA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 

RC SHINYANGA AWATAHADHALISHA WAHARIBIFU WA MISITU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telak akizungumza na watalaamu pamoja na wadau wa uhifadhi walioshiriki jana kwenye  kongamano ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani Kishapu.
 Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa akijibu hoja zilizotolewa na wadau mbalimbali  wa uhifadhi wa Misitu jana  wakati wa kongamano ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani Kishapu
 Mdau wa Uhifadhi wa Mazingira, Anna Matinye akichangia hoja  jana kwenye kongamano ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani Kishapu.
 Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa akiwasilisha maada   kwa wadau mbalimbali  wa uhifadhi wa Misitu kwa kuwasomea baadhi ya vipengele kwenye kitabu cha Sera ya Taifa ya Misitu  jana wakati wa kongamano ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani Kishapu
 Meneja wa Kanda ya Magharibi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Valentine Msusa  akijibu baadhi ya hoja za wadau kwenye kongamano ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani Kishapu
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telak ( wa tatu kushoto)  akiwa ameambatana na Kamati ya ulinzi na usalama wakiangalia baadhi ya miti iliyopandwa katika Shule ya Sekondari ya Kishapu inavyoendelea vizuri kabla ya kuanza kwa kongamano lililofanyika jana  ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani Kishapu
 Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa ( watatu kushoto) akiwa pamoja  na Mkurugenzi wa Rasilimali Misitu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Zawadi Mbwambo ( wapili kushoto) wakiandika baadhi  hoja zinazowatolewa na  wadau mbalimbali  wa uhifadhi wa Misitu  wakati wa kongamano ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani Kishapu
 Baadhi ya wadau wa uhifadhi wa Mazingira na Misitu wakifuatilia kongamano lililofanyika jana  ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani Kishapu
Mdau wa Uhifadhi wa Mazingira, Modestus Nyenza  akichangia hoja jana  kwenye kongamano ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani Kishapu.
Na Lusungu Helela-Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telak amewatahadhalisha wananchi kuwa yeyote atakayeharibu misitu kwa kukata au kuingiza mifugo kwenye  misitu atachukuliwa hatua za kisheria.
Akizungumza jana wilayani Kishapu  wakati wa  kongamano ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani humo,  Mkuu wa Mkoa  alipiga marufuku kukata miti bila ruhusa yake au ya Mkuu wa wilaya. 
Telak alisema marufu hiyo imekuja kwa kuchelewa kwa vile hatua iliyofikia  katika Wilaya hiyo  inatisha  hakuna mahindi yanayostawi kutokana  na  kutokuwa na  mvua ya kutosha. 
‘’Mtu yeyote atakayekata miti ajiandae kupelekwa jela  kwa vile kukata miti katika wilaya hii ni sawa na uuaji.’’ alisema Telak
Alifafanua kuwa mtu yeyote atakayetaka kukata miti hata ule uliopo uwanjani pake ni lazima aombe kibali kwa wahusika na atakayekiuka kukata bila kibali ajue jela inamwita.
 Wakati huo huo, Telak  alitoa agizo kwa wakuu wa wilaya wote kuhakikisha wanawakamata wale wote  watakaoingiza mifugo kwenye maeneo yaliyopandwa miti.
Aliongeza kuwa uharibifu wa misitu  unaoendelea kufanyika katika maeneo hayo  unazidi kuathiri hata  mifugo  kutokana na kukosekana kwa malisho kwa vile hakuna mvua inayonyesha.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Ezekiel Mwakalukwa  alisema suala la kulinda misitu linahitaji ushirikiano kutoka kwa jamii, wizara pekee haiwezi.
Alisema tatizo la uharibifu wa misitu katika wilaya ya Kishapu limechochea Idara kutengeneza kanzidata itakayosaidia kuzibana Halmashauri kujua imepanda miti mingapi na kati ya hiyo mingapi imepona. 
‘’Tunaanza  mwaka huu kukagua  ili kujua miti hiyo imepandwa wapi na maendeleo yake yakoje’’  alisisitiza  Mwakalukwa.
Amesema hali hiyo itasaidia kuthibiti Halmashauri ambazo zimekuwa zikitaja idadi kubwa ya miti iliyopandwa kila mwaka lakini miti hiyo imekuwa haionekani ikikua na pale unapohitaji kupelekwa ukaone miti hiyo  visingizio lukuki vimekuwa vikiibuka.

Maadhimisho ya wiki ya upandaji miti Kitaifa yanafanyika Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga ambapo kauli mbinu yake ni Tanzania ya kijani inawezekana panda miti kwa maendeleo ya viwanda

WAZIRI KIGWANGALLA KUONGOZA KILELE CHA MAADHIMISHO YA UPANDAJI MITI KITAIFA KESHO MKOANI SHINYANGA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

DC MATIRO APIGISHA KURA ZA SIRI KUBAINI WAUAJI WA WANAWAKE SHINYANGA VIJIJINI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Wananchi wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwasisitiza wananchi kutoa ushirikiano katika vyombo vya sheria ili kukomesha mauaji katika kata ya Salawe
Wananchi wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga

Na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Kufuatia kuibuka kwa taarifa za kuwepo kwa mauaji ya wanawake yanayoambatana na imani za kishirikina katika kata ya Salawe wilaya ya Shinyanga, mkuu wa wilaya hiyo Josephine Matiro amefanya mkutano na wananchi wa eneo hilo kwa ajili ya kutafuta chanzo na ufumbuzi kumaliza mauaji hayo.

Wananchi wa kijiji cha Songambele kata ya Salawe wanasema mauaji hayo yameanza kutokea tangu mwezi Desemba mwaka jana wakidai kuwa wanawake hukatwa mapanga ama kunyongwa na watu wasiofahamika ambao hutoweka na viungo vya siri vya wanawake wanaowaua. 

Inaelezwa kuwa katika kipindi cha  Januari Mosi hadi Machi 23 mwaka huu watu waliouawa katika kata hiyo ni wanne huku mauaji hayo yakihusishwa na imani za kishirikina.Kutokana na hali hiyo Mkuu wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya hiyo, alifika katika kata ya Salawe kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa mauaji hayo kwa njia ya kuwashirikisha wananchi.

Aidha baada ya kuzungumza na wananchi wa eneo hilo katika mkutano wa hadhara,mkuu huyo wa wilaya aliagiza kufanyika/kupigwa kwa kura za maoni kwa ajili ya kuwabaini wahusika wa mauaji hayo na kuondoka na kura hizo kwa ajili ya kuzifanyia kazi.

“Katika wilaya ya Shinyanga kuna kata 43, matukio ya mauaji ya namna hii yanatokea hapa,ni nyinyi hapa tu,sasa tumtafute mchawi na tumfanyie kazi,mkitaka kulimaliza tatizo hili ni  lazima mtupe ushirikiano,muwe tayari kufika mahakamani pale mtakapohitajika ,mjitokeze kutoa ushahidi ili wale watu msiwaone tena kwenye mitaa yenu”,alisema Matiro.

“Wananchi mmeendelea kulalamika kuwa kuna mauaji na kuitupia lawama serikali wakiwemo askari polisi kuwa wanapokea rushwa na kuwaachia huru watuhumiwa kumbe tatizo ni nyinyi kutotoa ushirikiano,naomba mbadilike, wafichueni wahusika ili tukomeshe tatizo hili kwani tunataka watu wawe salama na waishi kwa amani”,alieleza Matiro.

Aidha aliwataka viongozi wa serikali za mitaa na wananchi kwa ujumla kuacha kupokea wageni na kwamba wageni wote wajitambulishe ili kujua wanafanya nini na wametoka wapi ili kukomesha
Wakizungumza mbele ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga, wananchi hao walisema matukio hayo yanatishia usalama wao na kusababisha waishi kwa hofu.

Walisema mbali na kuishi kwa hofu pia wanashindwa kufanya kazi zao za maendeleo na uzalishaji mali.Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, ACP Simon Haule aliyekiri kuwepo kwa mauaji katika kata ya Salawe alisema chanzo ni kuwania mali,migogoro ya mashamba,wivu wa mapenzi na imani za kishirikina.

Aidha aliwataka wananchi kupuuza uzushi kwamba kwenye kata hiyo kuwa kuna watu wanakata mapanga wanawake na kisha kuondoka na sehemu zao nyeti yakiwemo matiti. 

“Kwenye mkoa wa Shinyanga hakuna kitu kama hicho, isipokuwa kuna takwimu za wananchi 27 kuuawa kwa kukatwa mapanga kutokana na sababu mbalimbali kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo kuanzia (2016- Machi 2018) ambapo wanawake 12, na wanaume 15. 

Alitaja takwimu za mauaji mkoa wa Shinyanga kwa kuchambua kila mwaka ambapo mwaka (2016) waliuawa watu 12, wanawake Sita, Wanaume Sita, (2017) wanaume nane, wanawake wanne, mwaka huu (2018) kuanzia Januari hadi Machi wanawake wawili na mwanaume mmoja jumla watu 27. 
 
Supported by Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa