Wenyeviti
wa mitaa ,vijiji na vitongoji Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
wamefanya sherehe ya kujipongeza kwa utendaji kazi wao wa miaka mitano.
Sherehe
hiyo imefanyika katika ukumbi wa chuo cha walimu Shinyanga ikiambatana
na zoezi la kuchangia damu katika benki ya damu iliyopo katika hospitali
ya Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga kwa lengo la kusaidia makundi
ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu wakiwemo wajawazito,watoto na
waathirika wa ajali.
Kwa
upande wake mgeni rasmi katika Sherehe hiyo Anord Makombe ambaye ni
mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga Mjini amewataka
wenyeviti hao kuendelea kufanya kazi kwa bidii ya kuwahudumia wananchi
katika kipindi hiki ambacho wanajiandaa na uchaguzi wa serikali za
mitaa.
Naye
mwenyekiti wa Mtaa wa Miti Mirefu Moke warioba ambaye pia ni mwenyekiti
wa wenyeviti wa serikali za mtaa Manispaa ya Shinyanga amewashukuru
wenyeviti kwa ushirikiano wao ambao wanaendelea kumpatia na kuomba
ushirikiano huo uendelee wakati wanapoendelea kuwatumikia na kutatua
kero za wananchi.
0 comments:
Post a Comment