Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab
Telack akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Kishapu(hawapo pichani)
wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya upandaji miti Kitaifa, ambayo mwaka
huu yamefanyika katika Wilaya ya Kishapu, Mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack (kulia) na Mkuu wa
Wilaya ya Kishapu Mhe. Nyabaganga Taraba wakiangalia viatu vya ngozi
vinavyotengenezwa na wajasiriamali Wilaya ya Kishapu katika maonesho ya
bidhaa mbalimbali ikiwa ni kuadhimisha siku ya upandaji miti Kitaifa.
Wakuu wa Mikoa ya Shinyanga na Tabora, Mhe. Zainab Telack na
Mhe. Aggrey Mwanri wakiangalia jiko rafiki la mazingira linalotumia
nishati ya mkaa kidogo katika maonesho ya bidhaa za misitu kwenye
maadhimisho ya upandaji Miti Kitaifa, Wilaya ya Kishapu.
Wakuu wa Mikoa ya Shinyanga na Tabora Mhe. Zainab Telack na
Mhe. Aggrey Mwanri wakitembelea maonesho katika maadhimisho ya upandaji
miti Kitaifa katika Wilaya ya Kishapu.
Viongozi na wananchi wa Kijiji cha Songwa, Wilaya ya Kishapu
wakipanda miti kando ya bwawa la Songwa ambalo lilikuwa hatarini kupotea
kutokana na kuvamiwa na shughuli za kilimo na mifugo na kukata
miti.Jumla ya miti 700 imepandwa kando ya bwawa hilo.
Sehemu ya wananchi wa kijiji cha Songwa, Wilaya ya Kishapu
waliojitokeza katika zoezi la upandaji miti kando kando ya bwawa la
Songwa, katika kuadhimisha upandaji miti Kitaifa, wakimsikiliza Mkuu wa
Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack.
Kutoka kushoto ni Mhe. Aggrey Mwanri, Mkuu wa Mkoa wa Tabora,
Mhe. Hamis Kigwangala, Waziri wa Maliasili na Utalii na Mhe. Zainab
Telack Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, baada ya kupanda mti na kuufunga kwa
njia ya umwagiliaji wa chupa, katika kilele cha maadhimisho ya Upandaji
miti Kitaifa tarehe 05 Aprili, 2018 katika Wilaya ya Kishapu.
0 comments:
Post a Comment