Benki
ya CRDB imeshiriki maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani (SUD)
duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Tabora katika Viwanja vya Ipuli.
Maadhimisho
hayo yaliyoanza tarehe 29 Juni 2024 na kuhitimishwa leo tarehe 6
Julai,2024 yalifunguliwa na Naibu Waziri wa Kilimo Mh. David Silinde na
kufungwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko.
Mkurugenzi
Mtendaji wa benki ya CRDB ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume
ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Abdulmajid Nsekela aliungana
na wafanyakazi wa Benki ya CRDB kutoka Makao Makuu wakiongozwa na Mkuu
wa Kitengo cha Kilimo Biashara, Maregesi Shaaban, pamoja na wafanyakazi
wa Kanda ya Magharibi wakiongozwa na Meneja wa Kanda hiyo, Jumanne
Wagana.
Benki
ya CRDB ikiwa ni mdau mkubwa wa sekta ya ushirika nchini, Benki ambayo
pia ndio mdhamini mkuu imetumia maadhimisho hayo kuonesha fursa za
uwezeshaji zinazotolewa kwa wateja wake waliopo kwenye mnyororo wa
thamani katika sekta za kilimo, uvuvi, ufugaji, viwanda na usafirishaji.
#CRDBBank
#UlipoTupo
0 comments:
Post a Comment