Afisa Afya wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu
Ndg.Mohamed Kiula, akieleza hali ya utekelezaji wa Kampeni ya Afya na usafi wa
mazingira katika wilaya ya Kishapu kwa wananchi na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Mhe.Ally N.Rufunga mapema wiki hii alipofanya ziara wilayani hapo katika
kijiji cha Bupigi kata ya Uchunga,kukagua utekelezaji wa kampeni hiyo ikiwa ni
maagizo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete
kuhamasisha jamii kubadili tabia na mtazamo wa jamii katika kutathmini suala la
usafi wa mazingira
Wananchi wa kijiji cha Bupigi kata ya Uchunga
wilaya ya Kishapu wakifanya zoezi la uchefuaji kwa kuongozwa na Afisa Afya wa
Halmashauri hiyo ili kuwahamaisha kubadili tabia ya kujisaidia vichakani hali
inayosababisha uchafuzi wa mazingira na hivyo kupata magonjwa ya milipuko kama
kuharisha, kipindupindu na matumbo
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Ally N. Rufunga
akiwaeleza umuhimu wa kutunza mazingira wananchi wa kijiji cha Bupigi wilaya ya
Kishapu mapema wiki hii alipotembelea kijijini hapo kuona utekelezaji wa
kampeni ya kitaifa ya Afya na usafi wa mazingira.
Baadhi ya wananchi katika kijiji cha
Nyamilangano wilaya ya Kahama wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga(hayupo
pichani),akiwaeleza umuhimu wa vyoo na usafi wa mazingira.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga aliyofanya kwenye
Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Halmashauri ya Mji Kahama pamoja na
Halmashauri ya wilaya ya Ushetu ametoa rai kwa wananchi kutizama upya suala la
mila na desturi kwa baadhi ya makabila kutotumia choo kimoja na wakwe
linasababisha uchafuzi wa mazingira kwani inabidi wakati fulani wakwe
kujisaidia vichakani pale wanapotembelewa na wakwe zao. Hivyo amewataka
wananchi kuacha mila hizo kwani hakuna madhara yoyote,vinginevyo kaya hizo ziwe
na vyoo viwili.
Amewataka pia viongozi hasa Wakuu wa wilaya kusimamia sheria ya
uchafu wa mazingira inayomfunga mtu yeyote mwenye kosa hilo kwa mwaka mmoja au
faini ya Tsh.Milioni moja.
Mkuu wa Mkoa ametembelea vijiji vya Bupigi wilaya ya Kishapu,
Mpunze Halmashauri ya wilaya ya Ushetu na Nyamilangano katika Halmashauri ya
Mji Kahama ili kuona hali ya utekelezaji wa kampeni hiyo.
Magdalena Nkulu
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Shinyanga
0 comments:
Post a Comment