Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Ally N. Rufunga amezindua Bodi mpya
ya Maji ya Mkoa wa Shinyanga katika halfa fupi iliyofanyika Alhamisi hii,
kwenye ofisi za Mamlaka ya Maji safi na maji Taka mkoani Shinyanga (SHUWASA).
Katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa amewataka wajumbe wa Bodi mpya
inayoongozwa na Mwenyekiti wake Brigedia Jenerali (Mstaafu),Dkt.Yohana Balele,kukabiliana
na changamoto mbalimbali zinazoikabili idara ya maji ambazo alizitaja kuwa ni
miundombinu hafifu hasa mabomba, uchache wa wateja wanaotumia maji na wateja
sugu wa kulipa madeni ya maji.
Wajumbe wengine wa bodi mpya ni Dkt.Anselm Tarimo (Katibu Tawala
Mkoa wa Shinyanga),Bw. Festo Kang'ombe ( Mkurugenzi wa Manispaa ya
Shinyanga),Dkt.Ramadhan Kabala(Mganga Mkuu wa Mkoa) na Bw.Fred
Shoo(Mfanyabiashara). Wengine ni Paulina M.Limbe,Mhe.Mourice Mugini,Dkt. Justus
Rwetabula na Sylivester Mahole ambaye ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na
Maji taka (SHUWASA)
Aidha, Mhe.Mkuu wa Mkoa amevunja bodi ya zamani ambayo imemaliza
muda wake baada ya kufanya kazi kwa miaka mitatu.
Katika hafla hiyo pia,Mkuu wa Mkoa amezindua baraza la Wafanyakazi
wa mamlaka ya Maji,amefungua tovuti ya Mamlaka ya maji safi na Maji taka
(SHUWASA) pamoja na kuzindua mkataba wa huduma kwa mteja.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya
Maji safi na Maji taka Mkoa wa Shinyanga Ndg. Sylivester Mahole akitoa taarifa
fupi ya Mamlaka hiyo kabla ya Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa kuzindua Bodi mpya ya
maji na kuvunjwa Bodi ya zamani
Akimpongeza Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Maji ya Mkoa wa Shinyanga
Brigedia Jenerali Mstaafu Dkt. Yohana Balele
Mkuu wa Mkoa akizindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa Mamlaka ya
Maji safi na Maji taka mkoani Shinyanga,kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Mhe.Anna Rose Nyamubi.
Mhe.Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally N.Rufunga akizindua tovuti ya Mamlaka ya Maji safi na Maji Taka Mkoani Shinyanga(SHUWASA)
Sura ya tovuti ya SHUWASA inavyoonekana baada ya kufunguliwa
Mkuu wa Mkoa Mhe.Rufunga akitoa nasaha kwa wajumbe wa bodi mpya ya
Maji ya Mkoa wa Shinyanga baada ya kuwakabidhi vitendea kazi.
0 comments:
Post a Comment