Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

 Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Shinyanga, 
ASF. Thomas Majuto, kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la 
Zimamoto na Uokoaji Tanzania, amevika vyeo askari watatu wa Mkoa 
wa Shinyanga kutoka cheo cha Koplo (CPL) hadi Sajini (SGT). 

Hafla hii ya kihistoria imefanyika leo katika kituo cha 
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Shinyanga.