Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telak akizungumza na watalaamu pamoja na
wadau wa uhifadhi walioshiriki jana kwenye kongamano ambalo lilikuwa ni
sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa
inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani Kishapu.
Mkurugenzi
wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa akijibu hoja
zilizotolewa na wadau mbalimbali wa uhifadhi wa Misitu jana wakati wa
kongamano ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji
miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani Kishapu
Mdau
wa Uhifadhi wa Mazingira, Anna Matinye akichangia hoja jana kwenye
kongamano ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji
miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani Kishapu.
Mkurugenzi
wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa akiwasilisha
maada kwa wadau mbalimbali wa uhifadhi wa Misitu kwa kuwasomea baadhi
ya vipengele kwenye kitabu cha Sera ya Taifa ya Misitu jana wakati wa
kongamano ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji
miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani Kishapu
Meneja
wa Kanda ya Magharibi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)
Valentine Msusa akijibu baadhi ya hoja za wadau kwenye kongamano ambalo
lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo
Kitaifa inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani Kishapu
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telak ( wa tatu kushoto) akiwa
ameambatana na Kamati ya ulinzi na usalama wakiangalia baadhi ya miti
iliyopandwa katika Shule ya Sekondari ya Kishapu inavyoendelea vizuri
kabla ya kuanza kwa kongamano lililofanyika jana ambalo lilikuwa ni
sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika
Mkoani Shinyanga wilayani Kishapu
Mkurugenzi
wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa ( watatu kushoto)
akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Rasilimali Misitu wa Wakala wa Huduma za
Misitu Tanzania (TFS) Zawadi Mbwambo ( wapili kushoto) wakiandika
baadhi hoja zinazowatolewa na wadau mbalimbali wa uhifadhi wa Misitu
wakati wa kongamano ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya
upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani
Kishapu
Baadhi
ya wadau wa uhifadhi wa Mazingira na Misitu wakifuatilia kongamano
lililofanyika jana ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya
upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani
Kishapu
Mdau
wa Uhifadhi wa Mazingira, Modestus Nyenza akichangia hoja jana kwenye
kongamano ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji
miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani Kishapu.
Na Lusungu Helela-Shinyanga
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telak amewatahadhalisha wananchi kuwa
yeyote atakayeharibu misitu kwa kukata au kuingiza mifugo kwenye misitu
atachukuliwa hatua za kisheria.
Akizungumza
jana wilayani Kishapu wakati wa kongamano ambalo lilikuwa ni sehemu
ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani
humo, Mkuu wa Mkoa alipiga marufuku kukata miti bila ruhusa yake au
ya Mkuu wa wilaya.
Telak
alisema marufu hiyo imekuja kwa kuchelewa kwa vile hatua iliyofikia
katika Wilaya hiyo inatisha hakuna mahindi yanayostawi kutokana na
kutokuwa na mvua ya kutosha.
‘’Mtu yeyote atakayekata miti ajiandae kupelekwa jela kwa vile kukata miti katika wilaya hii ni sawa na uuaji.’’ alisema Telak
Alifafanua
kuwa mtu yeyote atakayetaka kukata miti hata ule uliopo uwanjani pake
ni lazima aombe kibali kwa wahusika na atakayekiuka kukata bila kibali
ajue jela inamwita.
Wakati
huo huo, Telak alitoa agizo kwa wakuu wa wilaya wote kuhakikisha
wanawakamata wale wote watakaoingiza mifugo kwenye maeneo yaliyopandwa
miti.
Aliongeza
kuwa uharibifu wa misitu unaoendelea kufanyika katika maeneo hayo
unazidi kuathiri hata mifugo kutokana na kukosekana kwa malisho kwa
vile hakuna mvua inayonyesha.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Ezekiel
Mwakalukwa alisema suala la kulinda misitu linahitaji ushirikiano
kutoka kwa jamii, wizara pekee haiwezi.
Alisema
tatizo la uharibifu wa misitu katika wilaya ya Kishapu limechochea
Idara kutengeneza kanzidata itakayosaidia kuzibana Halmashauri kujua
imepanda miti mingapi na kati ya hiyo mingapi imepona.
‘’Tunaanza mwaka huu kukagua ili kujua miti hiyo imepandwa wapi na maendeleo yake yakoje’’ alisisitiza Mwakalukwa.
Amesema
hali hiyo itasaidia kuthibiti Halmashauri ambazo zimekuwa zikitaja
idadi kubwa ya miti iliyopandwa kila mwaka lakini miti hiyo imekuwa
haionekani ikikua na pale unapohitaji kupelekwa ukaone miti hiyo
visingizio lukuki vimekuwa vikiibuka.
Maadhimisho
ya wiki ya upandaji miti Kitaifa yanafanyika Wilayani Kishapu Mkoani
Shinyanga ambapo kauli mbinu yake ni Tanzania ya kijani inawezekana
panda miti kwa maendeleo ya viwanda
0 comments:
Post a Comment