RC TELACK AWASILISHA KILIO CHA UMEME KWA WAZIRI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu akitoa salamu kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack wakati alipomtembelea Ofisini kwake mapema leo.
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu na msafara wake, Ofisini kwake mapema leo.

MGODI WA EL HILLARY WAPEWA SIKU 14 KUJISAJILI MFUKO WA FIDIA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Antony Mavunde akitoa salam kwa uongozi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Shinyanga mara baada ya kuwasili Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Shinyanga. Kushoto aliyekaa ni Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko ambaye wameongozana katika ziara hiyo.
 Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Antony Mavunde (kushoto), Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko (kulia) wakiwa Ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Josephine Matiro walipofika kwa ajili ya kusaini kitabu cha wageni mapema jana.
 Naibu Waziri Mhe. Mavunde akitembelea mgodi wa almasi wa El Hillary baada ya kutoa maelekezo katika ziara yake mgodini hapo.

 Naibu Mawaziri wa Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Antony Mavunde (wa pili kushoto) na Madini Mhe. Dotto Biteko (katikati) wakitoa maelekezo kwa uongozi wa El Hillary mapema jana wakati wa ziara yao ya pamoja mgodini hapo.


NAIBU WAZIRI DK. NDUGULILE AFANYA ZIARA WILAYA YA SHINYANGA KUKAGUA HUDUMA ZA AFYA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amepiga marufuku dawa za serikali kuonekana zikiuzwa kwenye maduka ya watu binafsi kwani serikali haitaki kuingia kwenye matatizo ya uhaba wa dawa kwenye sehemu zake za kutolewa huduma ya afya.

NAIBU WAZIRI DK. NDUGULILE AZINDUA BARAZA LA WATOTO MKOA WA SHINYANGA,AKABIDHI OFISI,KOMPYUTA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile leo Jumatatu Februari 19,2018 amezindua Baraza la Watoto Mkoa wa Shinyanga na kukabidhi rasmi ofisi na kompyuta kwa ajili ya baraza hilo. 

NAIBU WAZIRI WA MADINI MHE BITEKO ATATUA MGOGORO WA LESENI YA MADINI ULIODUMU KWA MIAKA 10

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akihutubia mamia ya wachimbaji wadogo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mwazimba, Kata ya Chela, Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, Jana 3 Februari 2018. Picha zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua maeneo ya uchimbaji baada ya mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mwazimba, Kata ya Chela, Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, Jana 3 Februari 2018
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua maeneo ya wachimbaji wadogo wa chama cha ushirika cha Kasi Mpya Gold Mine katika Kijiji cha Mwazimba, Kata ya Chela, Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, Jana 3 Februari 2018
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akihutubia mamia ya wachimbaji wadogo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mwazimba, Kata ya Chela, Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, Jana 3 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua maeneo ya wachimbaji wadogo wa chama cha ushirika cha Kasi Mpya Gold Mine katika Kijiji cha Mwazimba, Kata ya Chela, Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, Jana 3 Februari 2018

Na Mathias Canal, Shinyanga

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ametatua mgogoro wa leseni uliodumu kwa takribani miaka kumi kwa kuamuru kupitia haraka eneo la leseni ya uchimbaji wa madini kwa wachimbaji wadogo wa chama cha ushirika cha Kasi Mpya Gold Mine.

Mhe Biteko ametoa agizo hilo Jana 3 Februari 2018 wakati akihutubia mamia ya wachimbaji wadogo waliohudhuria kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mwazimba, Kata ya Chela, Wilayani Kahama kufuatia malalamiko ya Mbunge wa Jimbo la Msalala Mhe Ezekiel Maige sambamba na malalamiko ya wachimbaji wadogo waliyoyawasilisha Wizara ya Madini Mjini Dodoma Januari 26, 2018.

Alisema kuwa wananchi walifunga safari mpaka ofisi za madini kwa ajili ya kupata uhalali wa kupimiwa eneo lao kwa kutumia GPS lakini Kaimu Afisa madini mkazi Wilaya ya Kahama akawabadilishia Nukta (Coordinator) ambazo baadaye zilionekana kuwa za eneo jingine ambalo ni mbuga isiyokuwa na madini huku eneo hilo likihamishiwa kwa ntu mwingine.

Mhe Biteko amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya madini Prof Simion Msanjila kumchukulia hatua za haraka za kinidhamu aliyekuwa Kaimu Afisa madini mkazi Wilaya ya Kahama aliyehusika na upotoshaji wa leseni na kuzua mgogoro wa usumbufu usiokuwa na sababu dhidi ya wananchi na serikali.

Alisema kuwa hakuna sababu ya Wizara ya Madini kukumbatia mgogoro huo wa leseni uliodumu kwa miaka kumi kwa sababu ya eneo ambalo lilipotoshwa na baadhi ya watendaji wa Wizara ya madini kwani jukumu la serikali ni kuwatumikia wananchi ikiwemo utatuzi wa kadhia mbalimbali zinazowakabili katika jamii.

Mhe Biteko kwa msisitizo mkubwa amewataka wachimbaji wadogo kuwa waaminifu na kufichua baadhi ya wachimbaji wanaoficha madini kwa kutorosha bila kulipa kodi kwani kufanya hivyo itakuwa njia pekee ya kuisaidia serikali na kuinusuru katika mtego wa wizi wa rasilimali hizo.

Ameongeza kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli haitawafumbia macho wamiliki wa leseni hizo ambao leseni zao zimedumu kwa muda mrefu bila kuzifanyia kazi kwani hawazalishi ajira yoyote wala kulipa kodi Hivyo serikali imekusudia kuzifuta na kuwapa watu wengine ambao watazifanyia kazi haraka iwezekanavyo ili kuongeza tija kwa sekta ya madini katika uchangiaji wa pato la Taifa.

Akitoa mfano katika eneo la Kahama kuna leseni 249 lakini zinazofanyiwa kazi ni 18 tu huku wenye leseni zisizofanya kazi wakisubiri wachimbaji wadogo wavumbue madini kisha huja kuwaondoa kwa kisingizio cha umiliki wa leseni. Leseni hizo zikiwa zimedumu kwa muda mrefu bila kuendelezwa.

Aidha,  alisema kuwa kuna maeneo makubwa manne ambayo yameshaamuliwa na serikali kutengwa kwa ajili ya wachimbaji wadogo ikiwemo eneo la Nyang'wale lenye hekari 996, eneo la Nyangarata lenye hekari 1074, Eneo la Buzwagi kilometa za mraba 53.4 na eneo la Kinamyuba kilomita za mraba 33.3

Alisema kuwa jukumu la serikali ni kutatua kero za wananchi sio kuwaongezea kero wananchi hivyo watendaji wote wa serikali wanapaswa kutimiza ndoto ya Rais Magufuli kwa kuwatumikia wananchi kwa imani na matendo imara kwa kuwanufaisha watumishi na rasilimali zao.

Sambamba na hayo Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko amewataka wananchi kuendelea na uchimbaji wakati taratibu zikifuatwa kukamilisha kumaliza mgogoro huo huku akiwahakikishia kutoondolewa tena na endapo kama watakuwa wanahitaji maeneo mengine yaliyotengwa kwa ajili ya wachimbaji wadogo wanapaswa kufuata taratibu za kisheria zilizoainishwa.

Awali mbunge wa Msalala Mhe. Ezekiel Maige alimweleza Mhe. Naibu Waziri kuwa watu wake wameonewa kwa muda mrefu na yeye akifuatilia mgogoro huo bila mafanikio.

"Ni kwasababu ya serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Magufuli kwa kimbilio la wanyonge, mheshimiwa Naibu Waziri nilikua nimekata tamaa" Alikaririwa Mhe Maige aliyekuwa akizungumza kwa hisia huku akishangiliwa na mamia ya wachimbaji wadogo waliokisanyika kwenye mkutano huo.

DC SHINYANGA AKABIDHI HUNDI ZA MIKOPO MIL 25 KWA VIKUNDI VYA VIJANA NA WANAWAKE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amekabidhi hundi za mikopo shilingi milioni 25 kwa vikundi vitatu vya vijana na kimoja cha wanawake zilizotolewa na halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

AGPAHI YAENDESHA WARSHA KWA WAVIU WASHAURI HALMASHAURI SITA ZA WILAYA MKOA WA SHINYANGA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI limeendesha warsha kwa WAVIU Washauri 75 kutoka halmashauri sita za wilaya mkoa wa Shinyanga ili kuwajengea uwezo kwa ajili ya kuboresha huduma katika vituo vya tiba na matunzo (CTC).

WAVIU washauri ni watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi na wamejiweka wazi na huru kuwashauri watu wanaoishi na VVU katika nyanja mbalimbali ikiwemo ufuasi mzuri wa dawa,kutoa ushauri nasaha kwa wenzao,kujitolea kufuatilia na kufundisha kwa njia ya ushuhuda wa maisha sambamba na kuhamasisha WAVIU wenzao kujiunga katika vikundi ili kusaidiana na kupunguza unyanyapaa.

Warsha hiyo ya siku tatu imeanza Jumatatu Januari 29,2018 katika ukumbi wa Karena Hotel Mjini Shinyanga na kukutanisha pamoja WAVIU Washauri takribani 75 kutoka halmashauri za wilaya za Kishapu, Manispaa ya Shinyanga, Shinyanga, Kahama Mji, Ushetu na Msalala.

Akizungumza katika warsha hiyo, Mratibu wa Masuala ya Watoto,Mama na Baba kutoka AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Aminael Tesha alisema lengo la warsha hiyo ni kuwajengea uwezo WAVIU Washauri ili waweze kuwaunganisha wateja kutoka kwenye jamii kwenda kwenye vituo vya tiba na matunzo na kuwafuatilia wateja waliopotea katika huduma na kuwarudisha kwenye huduma.

“Kupitia warsha hii tutapeana mikakati mbalimbali jinsi ya kuwatafuta wateja waliopotea katika huduma na kujadili namna ya kuboresha zaidi huduma katika vituo vya tiba na matunzo lakini pia kutoa elimu kuhusu haki za WAVIU Washauri”,alieleza Tesha.

Naye Mratibu wa Baraza la taifa la watu wanaoishi na VVU (NACOPHA), kanda ya Mwanza, Veronica Joseph aliwasihi watu wanaoishi na maambukizi ya VVU kujiweka wazi kwani itawasaidia kupata msaada kwa watu wanaowazunguka ikiwemo familia zao.

“Wale ambao hamjapima nawashauri mpime ili mjue afya zenu na ukibainika una maambukizi ya VVU jiweke wazi ili usaidiwe,kujiweka wazi kutakusaidia kuondoa matatizo na utaweza kupata fursa mbalimbali kutoka wafadhili”,alileleza.

Katika hatua nyingine alisema shirika la AGPAHI linatekeleza miradi ya Ukimwi katika mikoa sita nchini ambayo ni Shinyanga, Simiyu, Geita,Mwanza, Tanga na Mara kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania kwa ufadhili wa serikali ya Watu wa Marekani kupitia Centres for Disease Control and Preventation (CDC).
Mratibu wa Masuala ya Watoto,Mama na Baba kutoka AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Aminael Tesha akizungumza wakati wa warsha ya siku tatu ya WAVIU Washauri halmashauri sita za wilaya mkoa wa Shinyanga iliyofanyika katika ukumbi wa Karena Hotel Mjini Shinyanga.
Aminael Tesha akielezea malengo ya warsha hiyo.
Mwezeshaji katika warsha hiyo, Veronica Joseph ambaye ni Mratibu wa Baraza la taifa la watu wanaoishi na VVU (NACOPHA), kanda ya Ziwa, akielezea kuhusu umuhimu wa watu wanaoishi na maambukizi ya VVU kuwa wafuasi wazuri wa dawa za kufubaza makali ya VVU na kujiweka wazi.
MVIU Mshauri, Joyce Philimon kutoka mkoani Simiyu ambaye anaishi na maambukizi ya VVU tangu mwaka 1997 akielezea umuhimu wa kujiweka wazi pale unapobaini kuwa umepata maambukizi ya VVU. Kujiweka wazi kwa Joyce kumfanya aishi salama na kwa amani na kupata fursa za kushiriki shughuli mbalimbali kutoka kwa wadau. 
MVIU Mshauri Seleman Habibu kutoka Kahama akielezea namna alivyoweza kuishi na maambukizi ya VVU tangu mwaka 2000 na ana watoto wawili ambao hawana maambukizi ya VVU na mke wake pia hana maambukizi ya VVU.
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Watu Wanaoishi na VVU katika Manispaa ya Shinyanga,Vedastus Mutangira akizungumza katika warsha hiyo ambapo akiwasisitiza watu wanaoishi na VVU kumeza dawa kwa utaratibu sahihi uliowekwa pamoja na kuhudhuria kliniki mara kwa mara.
WAVIU Washauri wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yanajiri ukumbini.
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini.
Mwezeshaji katika warsha hiyo,Vedastus Mutangira akitoa elimu kuhusu VVU na Ukimwi. Aliwasisitiza watu wanaoishi na VVU kumeza dawa kwa utaratibu sahihi uliowekwa pamoja na kuhudhuria kliniki mara kwa mara.
MVIU Mshauri Neema Anthony kutoka kutoka CTC ya Segese katika halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga akichangia hoja wakati wa warsha hiyo.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa