Wananchi wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwasisitiza wananchi kutoa
ushirikiano katika vyombo vya sheria ili kukomesha mauaji katika kata ya
Salawe
Wananchi wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Kufuatia
kuibuka kwa taarifa za kuwepo kwa mauaji ya wanawake yanayoambatana na
imani za kishirikina katika kata ya Salawe wilaya ya Shinyanga, mkuu wa
wilaya hiyo Josephine Matiro amefanya mkutano na wananchi wa eneo hilo
kwa ajili ya kutafuta chanzo na ufumbuzi kumaliza mauaji hayo.
Wananchi
wa kijiji cha Songambele kata ya Salawe wanasema mauaji hayo yameanza
kutokea tangu mwezi Desemba mwaka jana wakidai kuwa wanawake hukatwa
mapanga ama kunyongwa na watu wasiofahamika ambao hutoweka na viungo vya
siri vya wanawake wanaowaua.
Inaelezwa kuwa katika
kipindi cha Januari Mosi hadi Machi 23 mwaka huu watu waliouawa katika
kata hiyo ni wanne huku mauaji hayo yakihusishwa na imani za
kishirikina.Kutokana
na hali hiyo Mkuu wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ambaye ni
mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya hiyo, alifika katika
kata ya Salawe kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa mauaji hayo kwa njia ya
kuwashirikisha wananchi.
Aidha
baada ya kuzungumza na wananchi wa eneo hilo katika mkutano wa
hadhara,mkuu huyo wa wilaya aliagiza kufanyika/kupigwa kwa kura za maoni
kwa ajili ya kuwabaini wahusika wa mauaji hayo na kuondoka na kura hizo
kwa ajili ya kuzifanyia kazi.
“Katika
wilaya ya Shinyanga kuna kata 43, matukio ya mauaji ya namna hii
yanatokea hapa,ni nyinyi hapa tu,sasa tumtafute mchawi na tumfanyie
kazi,mkitaka kulimaliza tatizo hili ni lazima mtupe ushirikiano,muwe
tayari kufika mahakamani pale mtakapohitajika ,mjitokeze kutoa ushahidi
ili wale watu msiwaone tena kwenye mitaa yenu”,alisema Matiro.
“Wananchi
mmeendelea kulalamika kuwa kuna mauaji na kuitupia lawama serikali
wakiwemo askari polisi kuwa wanapokea rushwa na kuwaachia huru
watuhumiwa kumbe tatizo ni nyinyi kutotoa ushirikiano,naomba mbadilike,
wafichueni wahusika ili tukomeshe tatizo hili kwani tunataka watu wawe
salama na waishi kwa amani”,alieleza Matiro.
Aidha
aliwataka viongozi wa serikali za mitaa na wananchi kwa ujumla kuacha
kupokea wageni na kwamba wageni wote wajitambulishe ili kujua wanafanya
nini na wametoka wapi ili kukomesha
Wakizungumza
mbele ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga, wananchi hao walisema matukio
hayo yanatishia usalama wao na kusababisha waishi kwa hofu.
Walisema
mbali na kuishi kwa hofu pia wanashindwa kufanya kazi zao za maendeleo
na uzalishaji mali.Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,
ACP Simon Haule aliyekiri kuwepo kwa mauaji katika kata ya Salawe
alisema chanzo ni kuwania mali,migogoro ya mashamba,wivu wa mapenzi na
imani za kishirikina.
Aidha
aliwataka wananchi kupuuza uzushi kwamba kwenye kata hiyo kuwa kuna
watu wanakata mapanga wanawake na kisha kuondoka na sehemu zao nyeti
yakiwemo matiti.
“Kwenye
mkoa wa Shinyanga hakuna kitu kama hicho, isipokuwa kuna takwimu za
wananchi 27 kuuawa kwa kukatwa mapanga kutokana na sababu mbalimbali kwa
kipindi cha miaka mitatu mfululizo kuanzia (2016- Machi 2018) ambapo
wanawake 12, na wanaume 15.
Alitaja
takwimu za mauaji mkoa wa Shinyanga kwa kuchambua kila mwaka ambapo
mwaka (2016) waliuawa watu 12, wanawake Sita, Wanaume Sita, (2017)
wanaume nane, wanawake wanne, mwaka huu (2018) kuanzia Januari hadi
Machi wanawake wawili na mwanaume mmoja jumla watu 27.
0 comments:
Post a Comment