Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu akitoa salamu kwa Mkuu wa
Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack wakati alipomtembelea Ofisini kwake
mapema leo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza na Naibu
Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu na msafara wake, Ofisini kwake
mapema leo.
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amewasilisha changamoto ya
kukosekana umeme wa uhakika katika baadhi ya maeneo Mkoani hapa kwa
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu (MB) mapema leo, Ofisini
kwake.
Mhe.
Telack amesema kuwa kwa upande wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
na Mji wa Kahama suala la umeme bado ni changamoto kwani sehemu za
pembezoni hakuna umeme wakati ni umbali mdogo kutoka katikati ya mji.
Amemuomba
Mhe. Naibu Waziri kuliangalia suala hilo na kumuhakikishia kuwa, iwapo
kutakuwa na umeme pembezoni mwa miji hii, Shirika la umeme TANESCO
litaongeza mapato yake ya kila mwezi kutokana na kuongezeka kwa matumizi
ya umeme, aidha itasaidia kukuza uwekezaji wa shughuli mbalimbali na
kuongeza uchumi.
Aidha,
Mhe. Telack ameutaka uongozi wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga kuwasikiliza
wananchi na kushirikiana na Ofisi yake wakati wowote kwa masuala
mbalimbali kwa lengo la kuwasaidia wananchi wa Mkoa wa Shinyanga.
Mhe.
Naibu Waziri Subira Mgalu amepita Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
kwa lengo la kumsalimia baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua
utekelezaji wa miradi ya REA Mkoani hapa.
Na Magdalena Nkulu
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
0 comments:
Post a Comment