Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Antony Mavunde (kushoto), Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko (kulia) wakiwa Ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Josephine Matiro walipofika kwa ajili ya kusaini kitabu cha wageni mapema jana.
Naibu Waziri Mhe. Mavunde akitembelea mgodi wa almasi wa El Hillary baada ya kutoa maelekezo katika ziara yake mgodini hapo.
Naibu Mawaziri wa Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Antony Mavunde (wa pili kushoto) na Madini Mhe. Dotto Biteko (katikati) wakitoa maelekezo kwa uongozi wa El Hillary mapema jana wakati wa ziara yao ya pamoja mgodini hapo.
****************
Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Antony Mavunde ametoa siku 14
kwa Mkurugenzi wa Mgodi wa Almasi wa El – Hillary uliopo Wilaya ya
Kishapu Mkoani Shinyanga, kujisajili katika mfuko wa fidia kwa watumishi
(WCF) na kulipa faini kwa kuchelewesha malipo ya usajili.
Mhe. Mavunde ametoa agizo hilo mapema Jumanne hii alipofanya ziara ya
kushtukiza mgodini hapo, akiambatana na Naibu Waziri wa Madini Mhe.
Dotto Biteko kwa lengo la kufuatilia hatua za utekelezaji wa agizo la
Serikali lililowataka waajiri wote kujisajili katika mfuko wa fidia
ifikapo tarehe 30 Septemba, 2017.
Amesema Serikali, pamoja na kulinda maslahi ya watumishi, pia ina nia
njema ya kuwapunguzia waajiri jukumu la kuwahudumia watumishi walioumia
kazini.
Mavunde amewataka waajiri kuwa na utamaduni wa kutii sheria zilizowekwa
siyo hadi kusikia Waziri anakuja kufuatilia ndiyo wanalipa fidia hiyo.
Aidha, Mhe. Mavunde ameutaka uongozi wa mgodi huo kufuatilia maelekezo
ya Ofisi ya Kazi Mkoa, kuhakikisha inawapatia watumishi wake zaidi ya
160 mikataba ya kazi inayokidhi matakwa ya kisheria.
Na Magdalena Nkulu
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Shinyanga
0 comments:
Post a Comment