Hatua hiyo imeazimiwa
na kikao cha kamati za ulinzi na usalama za mikoa ya Shinyanga na Tabora
kilichofanyika jana katika kijiji cha Magogo ambako vurugu hizo zimetokea.
Wakitoa taarifa baada
ya kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally N. Rufunga na Mkuu wa Mkoa
wa Tabora Bi. Fatuma Mwasa wamesema pamoja na kuundwa tume hiyo kikao
kimeazimia kuwa, wafugaji walioko katika kijiji cha Magalata wilayani Kishapu
mkoa wa Shinyanga wabaki kwenye eneo lao na wasivuke mto Manonga kulisha
ng'ombe wao..
Pia, wakulima walioko
katika vijiji vya Magogo na Isakamaliwa wilaya ya Igunga mkoani Tabora wabaki
huko na wasivuke mto Manonga.
Aidha,wakulima
walioharibiwa makazi waendelee na shughuli zao kama kawaida katika vijiji vya Magogo
na Isakamaliwa mkoani Tabora aidha,ulinzi wa wananchi wa vijiji vya Magogo na
Isakamaliwa unaimarishwa, askari polisi wameongezwa ili kuhakikisha usalama wa
eneo hilo
Kikao pia kimeazimia
waharibifu wa makazi ya watu na wauaji wakamatwe ndani ya siku saba.
Azimio lingine ni
kamati zote mbili kutoa Elimu kwa wananchi wa vijiji vya Magalata wilaya ya
Kishapu na Magogo na Isakamaliwa wilaya ya Igunga, vilevile Halmashauri zote
mbili za Igunga na Kishapu zihakikishe zinaboresha sheria ndogo ili kuwaadhibu
wanaokiuka utaratibu wa mipaka.
Kwa pamoja,
Mhe.Rufunga na Mhe. Mwasa wamesema serikali imelaani vikali vitendo hivyo
vilivyofanywa na wafugaji wa jamii ya Kitaturu na kusema ni vitendo
visivyovumilika kwani siyo desturi ya Watanzania hivyo serikali imetoa salamu
za pole kwa wafiwa na itahakikisha majeruhi mmoja anahudumiwa na pia watuhumiwa
lazima wakamatwe.
Na Magdalena Nkulu
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Shinyanga
0 comments:
Post a Comment