SHULE ZATAKA PEDI KWA AJILI YA WANAFUNZI WA KIKE SHINYANGA,DC AOMBA MSAMAHA WA KODI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Pamoja na jitihada zinazofanyika kuhakikisha kuwa na vyumba maalum kwa ajili ya watoto wa kike kujisitiri wanapokuwa katika hedhi lakini bado changamoto kubwa ni upatikanaji wa vitambaa wakati wa hedhi "pedi"kwa watoto wa kike hasa kwa watoto wasio na uwezo.

UFAFANUZI WA ACACIA DHIDI YA TUHUMA ZA USAFIRISHAJI WA MAKINIKIA YA DHAHABU/SHABA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
Zimepita wiki tatu (3), tangu kutangazwa kwa zuio la ghafla la ushafirishaji wa makinikia ya dhahabu/shaba lililotangazwa tarehe 2 Machi. Tangu kutangazwa kwa zuio hilo kumekua na upotoshwaji mkubwa wa taarifa kwenye vyombo mbalimbali vya habari. Hadi sasa, Acacia haikutoa tamko lolote hadharani, sababu tumekua tukielekeza jitihada katika kutafuta muafaka na Serikali juu ya nini kifanyike. Lakini, kutokana na kiwango kikubwa cha taarifa potofu na zisizo sahihi zenye uvumi mwingi ambao unaweza kutuletea taswira mbaya kwa kampuni, kwa wafanyakazi wetu na pia kwa Tanzania kwa ujumla, tumeamua kuweka wazi hali halisi juu ya hoja mbalimbali. Acacia inapinga vikali kuhusika na madai yaliyotolewa mwishoni mwa wiki wakati wa ziara ya ukaguzi bandarini – Dar es Salaam kwamba sisi tulikua tukifanya njama za kutorosha makontena yenye makinikia ya dhahabu/shaba nje ya nchi licha ya katazo lililotangazwa na Serikali. Ukweli ni kwamba si Acacia wala wateja wetu walijaribu kusafirisha makinikia haya nje ya nchi. Kabla ya kutangazwa kwa zuio hilo, makontena, 256 ambayo sasa yamehifadhiwa ZamCargo (zamani ikijulikana kama Mofed - ambaye ni wakala wa usafirishaji wa forodha Customs Freight Services, CFS) yalikuwa tayari yamesafirishwa kutoka migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi, na makontena mengine 21 yaliyokutwa katika bandari ya Dar es Salaam yakiwa tayari yameidhinishwa na idara ya forodha ya Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) na yalikua tayari kusafirishwa. Zoezi hili huwa linajumuisha TRA pamoja na Wizara ya Nishati na Madini (MEM) ambao kwa pamoja wanahusika katika mchakato wa kusafirisha mikinikia nje ya nchi kwa utaratibu maalum. Acacia imekuwa ikisafirisha makinikia nje ya nchi kutoka mgodi wa Bulyanhulu tangu mwaka 2001 na kutoka mgodi wa Buzwagi tangu mwaka 2010 huku ikiweka bayana mapato yote yanayohusiana na makinikia ya dhahabu/Shaba na kuwasilisha Serikalini. Mapato haya pia yamekua yakitolewa kama mrahaba na malipo mengine kama kodi ya mapato kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Sheria za Tanzania zinaruhusu migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi kuuza nje ya nchi makinikia ya dhahabu/Shaba, sambamba na kusafirisha makinikia ndani ya makontena. Migodi hii imekua makini kukidhi vigezo vyote vya kisheria na matakwa ya vibali vya usafirishaji (Export Permits). Tunapenda umma ufahamu kua kila kitu tunachokifanya kinathibitishwa na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA). Kila kontena la makinikia linalosafirishwa linachukuliwa sampuli chini ya uangalizi wa idara zote za usimamizi ambazo ni TMAA na Kampuni ya huduma za maabara (SGS) ili kwamba Acacia na Serikali ziweze kukadiria wingi wa madini ya dhahabu, shaba na fedha yaliyomo. Matokeo ya sampuli hizi hupelekwa TMAA, TRA, Acacia na kampuni zenye mitambo maalum ya kuyeyusha na kuchenjua makinikia (Smelters) ili kubaini mrahaba wa awali ambao Serikali italipwa kabla ya kusafirisha makinikia. Ni pale tu ambapo upimwaji wa sampuli umekamilika, na mrahaba umeshalipwa kwa Serikali, ndipo makontenta yanafungwa kwa lakiri maalum za TMAA, MEM na TRA, na makinikia yanaweza kusafirishwa kutoka migodini. Kisha makontena husafirishwa wa magari ya kubebea mizigo hadi kituo cha forodha cha Isaka ambako nyaraka za mwisho za kusafirisha nje ya nchi hutolewa na MEM pamoja na TRA, na makontena kuidhinishwa kwa safari ya kwenda bandari ya Dar es Salaam. Baada nyaraka zote kukaguliwa na kuhakikishwa na maafisa wa forodha, kila kontena hukaguliwa kwa kutumia mtambo maalumu wa kieletroniki (Scanner) ili kuthibitisha kua ndani yake hakuna kitu kingine chochote isipokua makinikia ya dhahabu/Shaba tu. Baada ya hapo makontena huhifadhiwa chini ya ulinzi wa maafisa wa forodha mpaka hatua za mwisho za upakiaji wa makontena kwenye meli tayari kwa kusafirisha nje ya nchi. Acacia iko tayari kushirikiana na Serikali kutafiti uwezekano wa Tanzania kua na kiwanda cha uchenjuaji ambacho kitatoa ajira na kuleta maendeleo kwenye sekta hii. Maendeleo ya teknolojia yanaweza kutoa muelekeo stahili juu ya uwezekano huu. Hadi hivi sasa, migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi imeendelea na uzalishaji kama kawaida hata baada ya zuio la Serikali na makinikia haya yamehifadhiwa katika maeneo maalumu migodini. Lakini hali hii haiwezi kua ya kudumu kutokana na umuhimu wa kukusanya mapato yatokanayo na biashara ya makinikia kwa migodi hii miwili. Acacia inaunga mkono kikamilifu jitihada za bila kuchoka za Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali yake kuwekeza katika maendeleo ya nchi kupitia elimu, ajira na viwanda. Acacia ni mwajiri mkubwa nchini Tanzania na sasa tumetoa ajira za moja kwa moja za zaidi ya wafanyakazi 5,000 pamoja na wakandarasi na ajira zingine 55,000 katika uchumi, zinazofaidisha familia na jamii kwa ujumla. Kati ya waajiriwa wote wa Acacia, zaidi ya asilimia 96 ni Watanzania. Migodi yetu inasaidia kuendeleza wazawa kupitia idara yetu ya ugavi ili kuwapatia fursa endelevu za kibiashara. Tunapenda kuendelea kuwakaribisha maafisa wa serikali kuja kutembelea migodi yetu ili waweze kufahamu mchakato mzima wa kuzalisha madini, kukusanya sampuli na kusafirisha makinikia ya dhahabu/shaba nje ya nchi.

CHAMA CHA WATU WENYE UALBINO CHATOA ELIMU MASUALA YA UALBINO KANISA KUU LA KKKT SHINYANGA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Chama cha watu wenye ualbino nchini (Tanzania Albinism Society-TAS) kimeanza kampeni ya kutoa elimu kuhusu masuala ya ualbino katika nyumba za ibada ambapo leo viongozi wa chama hicho taifa wametoa elimu katika kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria lililopo mjini Shinyanga.

MAADHIMISHO YA SIKU YA KIFUA KIKUU DUNIANI MKOA WA SHINYANGA YAFANYIKA KWENYE MACHIMBO YA NYANGARATA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu Duniani “World TB Day” mkoa wa Shinyanga yamefanyika katika machimbo ya dhahabu ya Nyangarata kata ya Lunguya halmashauri ya Msalala wilayani Kahama.

Tigo, RITA kuanza awamu ya nne usajili wa watoto Geita, Shinyanga

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dr Harrison Mwakyembe akionesha mojawapo ya simu 800 zilizotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo ili kufanikisha zoezi la usajili na utoaji wa vyeti kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano, uzinduzi wa zoezi hilo kwa awamu ya tatu ulifanyika Septemba  mwaka jana mjini Iringa. Kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza.
Na Mwandishi wetu.
Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo kwa kushirikiana na Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi (RITA)pamoja na UNICEF inategemea kuzindua awamu ya nne ya usajili wa watoto chini ya miaka mitano katika mikoa ya Geita na Shinyanga mapema wiki ijayo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na RITA, Mpango huu wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka mitano unatarajiwa kutekelezwa katika wilaya zote tatu (3) zilizo na halmashauri 6 za mkoa wa Shinyanga na Wilaya zote tano (5) zilizo na halmashauri sita (6) katika mkoa wa Geita.

“Kwa mujibu wa takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, ni asilimia 9.4 ya watoto wa mkoa wa Shinyanga na asilimia 8.6 katika mkoa wa Geita wamesajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa. Lengo la RITA mara itakapoanza kutekeleza mpango huu ni kusajili watoto wote 740,912 ambao hawajasajiliwa na hawana vyeti vya kuzaliwa katika mikoa yote miwili kwa kipindi cha miezi 6,” alisemakaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Rita Emmy Hudson.

Ili kufanikisha utekelezaji mpango huu kutakuwa na vituo vya usajili zaidi ya 650 vitakavyokuwa na wasajili wasaidizi wapatao 1,250 kwa mikoa yote miwili. Wasajili hawa watawekwa katika ofisi za afisa mtendaji wa mtaa na vile vile katika maeneo ambayo kinamama huenda kupata huduma za kiafya za watoto.

“Matokeo tuliyoyapata mwaka jana katika utekelezaji wa mpango huu katika mikoa ya Iringa na Njombe yatatumika kuhakikisha watoto wote wanapata huduma hii katika mikoa ya Geita na Shinyanga,” alisema Hudson huku akiongeza kwamba mikoa hiyo iliweza kusajili watoto kwa asilimia mia moja (100%) kwa kipindi cha miezi mitano huko Iringa na Njombe.

Meneja wa Huduma za Jamii wa kampuni ya Tigo, Halima Okash alisema kampuni ya Tigo imekuwa mshirika mkuu wa mkakati wa Usajili wa Watoto wa chini ya miaka mitano toka mwaka 2012 ili kuiwezesha serikali kupunguza tatizo la muda mrefu la watoto kutosajiliwa na mamlaka husika pindi wanapozaliwa hivyo kuathiri mipango ya maendeleo ya muda mfupi na ile ya muda mrefu.
“Duniani kote takwimu sahihi na zinazopatikana kwa wakati ni jambo muhimu ili kufanikisha mipango mbalimbali ya maendeleo ndio maana kati ya malengo makuu ya mkakati huu ni kutumia teknolojia ya simu za kiganjani katika kuchukua na kutuma taarika kwenda katika kanzidata (database) ya RITA mara mtoto anaposajiliwa kwenye vituo vilivyoaainishwa,” alisema Okash.
Okash aliongeza kwamba kampuni ya simu za mkononi ya Tigo inajivunia kuweza kutumia rasilimali ya ujuzi tulio nao katika kuwezesha kila mtoto nayezaliwa kutambuliwa na mamlaka husika hivyo serikali kufahamu kuna watoto kiasi gani katika umri fulani.
Cheti cha kuzaliwa ni nyaraka ya awali ya utambulisho kwa mtoto inayomwezesha kutambuliwa uwepo wake na ni haki ya mtoto ya msingi. Hudson aliwaomba wadau wote ikiwa pamoja na viongozi wa mikoa, wilaya, halmashauri, tarafa, kata, mitaa/vijiji na vitongoji kushirikiana kwa pamoja ili kuweza kufanikisha utekelezaji wa mpango huu.

“Vilevile,tunawaomba Viongozi wa dini, wanasiasa, wanahabari na viongozi wa jadi ambao watusaidia kuelimisha wananchi kuhusu kujitokeza kwa wingi kuwasajili watoto ili wapate vyeti vya kuzaliwa,” alisema Hudson.
Mwisho.

WADAU WA ZAO LA MKONGE WAFANYA MKUTANO SHINYANGA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Alhamis ,Machi 16,2017 kumefanyika Mkutano wa wadau wa zao la mkonge kutoka wilaya ya Meatu mkoa wa Simiyu na wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga.

JUMLA YA WANAFUNZI 228 WAONWA, BUHANGIJA MKOANI SHINYANGA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Daktari wa Kinywa na Meno Hospitali ya Huruma CDH  ya Mkoani Kilimanjaro Sr,  Benjamine Buya (kushoto) akimfanyia uchunguzi wa Afya ya Kinywa na Meno Mwanafunzi wa Darasa la 3 wa Shule ya Msingi Jumuishi ya Buhangija Mkoani Shinyanga, Tausi  Yanssni , anayeshuhudia (katikati) ni Mwalimu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Profesa Bakari Lembariti 
 Daktari wa Kinywa na Meno Hospitali ya Huruma CDH  ya Mkoani Kilimanjaro Sr,  Benjamine Buya (kushoto) akimfanyia uchunguzi wa Afya ya Kinywa na Meno Mmoja wa wanafunzi wanaosoma katika Shule hiyo jana
Maktari Bingwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Habiba Madjapa (kushoto) akimfanyia uchunguzi wa Afya ya Kinywa na Meno mwanafunzi wa Shule hiyo, kulia ni Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno, Tanzania Dr. Lorna Carneiro
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Jumuishi ya Buhangija Mkoani Shinyanga wakipiga mswaki mara baada ya kufanyiwa uchunguzi wa Afya ya Kinywa na Meno
 Wanafunzi Wenye ulemavu wa kutosikia wakizungumza jambo wakati Madaktari wa Afya na  Kinywa na Meno walipokuwa wakifanya uchunguzi wa Afya ya Kinywa na Meno katika Shule ya Buhangija mkoani Shinyanga
Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania, Dr. Lorna Carneiro (wa pili kushoto) akizungumza jambo na mtoto  moja ambaye anasoma katika Shule hiyo,
 Na Khamis Mussa, Shinyanga.
 ambapo aliweza kusema, napenda kuwashukuru wenyeji wetu kwa ushirikiano waliotupa na kuwashukuru madaktari wote waliojitokeza katika kusaidia kutowa huduma kwa watoto wote na kwa jamii nzima bila kuchoka nakuwaomba wahisani kujitokeza  kusaidia kupambana na magonjwa ya Kinywa na Meno kwa watoto hao, Carneiro alisema, amepata faraja yakuona tofauti ya watoto hao ni kubwa sana tofauti na mwaka wakwanza walipofika Kituoni hapo.
Kadri wanavyo endelea kuja anaona afya za watoto hao zinazidi kuimarika kutokana na Elimu wanayoendelea kuitoa kwa watoto hao kwa utumiaji na upigaji mswaki,  inaonyesha elimu wanayoendelea kuitowa inazingatiwa katika utunzaji wa afya ya kinywa na meno na elimu wanayoendelea kuitowa ina wasaidia katika utunzaji wa hali ya afya zao za kinywa na meno, 
Carneiro aliendelea kusema, MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana anatarajiwa kuongoza 
matembezi ya Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno yatakayofanyika mkoani humo Machi 19 mwaka huu.Matembezi hayo yatafanyika katika Viwanja vya Nyerere Square na uwashirikisha wadau mbalimbali wa sekta ya afya na wananchi wa mkoa huo kwa kupata huduma ya afya ya kinywa na meno bure . aliesma
wamepanga kuwa na matembezi ya uhamasishaji wa jamii kuhusu umuhimu 
wa afya ya kinywa na Meno tarehe 19 Machi, eneo ya Nyerere Square, Dodoma. 
Sanjari na matembezi hayo siku itakayofuata Machi 20, ambayo itakuwa ni kilele cha wiki ya Afya ya Kinywa na Meno Tanzania na Siku ya Afya ya Kinywa na Meno Duniani, kutakuwa na uchunguzi wa afya ya kinywa ya meno kwa wananchi bila malipo na katika maadhimisho hayo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa  ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi, George Simbachawene.
 Mkuu wa Kituo ambaye ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Buhangija Seleman Kipanya, akieleza hali ilivyokuwa kabla ya jopo la Madaktari  kufika na kutowa elimu ya Afya ya Kinywa na Meno kwakuwachunguza na kutibu watoto waliogundulika na matatizo mbalimbali, aliyasema hayo, Kipanya, wakati wa Wiki ya Kinywa na Meno kwa
Mwanzoni katika mwaka wa kwanza kulikuwa na matatizo mengi ambayo yaliyokuwa yanawakabili vijana ikiwa ni pamoja na kutoboka kwa meno ambapo hawakuwa na namnabora ya kusafisha meno , lakini kwa mwaka wa kwanza baada ya kutowa elimu ya kinywa na kuwafanyia uchunguzi na kutowa ushauri na mwaka uliofatia kulikuwa na mabadiliko makubwa na kwamwaka huu tulionao kiukweli kumekuwa na mabadiliko makubwa sana
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa