Shirika
la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI)
linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI
limeendesha warsha kwa WAVIU Washauri 75 kutoka halmashauri sita za
wilaya mkoa wa Shinyanga ili kuwajengea uwezo kwa ajili ya kuboresha
huduma katika vituo vya tiba na matunzo (CTC).
WAVIU
washauri ni watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi na
wamejiweka wazi na huru kuwashauri watu wanaoishi na VVU katika nyanja
mbalimbali ikiwemo ufuasi mzuri wa dawa,kutoa ushauri nasaha kwa
wenzao,kujitolea kufuatilia na kufundisha kwa njia ya ushuhuda wa maisha
sambamba na kuhamasisha WAVIU wenzao kujiunga katika vikundi ili
kusaidiana na kupunguza unyanyapaa.
Warsha
hiyo ya siku tatu imeanza Jumatatu Januari 29,2018 katika ukumbi wa
Karena Hotel Mjini Shinyanga na kukutanisha pamoja WAVIU Washauri
takribani 75 kutoka halmashauri za wilaya za Kishapu, Manispaa ya
Shinyanga, Shinyanga, Kahama Mji, Ushetu na Msalala.
Akizungumza
katika warsha hiyo, Mratibu wa Masuala ya Watoto,Mama na Baba kutoka
AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Aminael Tesha alisema lengo la warsha hiyo ni
kuwajengea uwezo WAVIU Washauri ili waweze kuwaunganisha wateja kutoka
kwenye jamii kwenda kwenye vituo vya tiba na matunzo na kuwafuatilia
wateja waliopotea katika huduma na kuwarudisha kwenye huduma.
“Kupitia
warsha hii tutapeana mikakati mbalimbali jinsi ya kuwatafuta wateja
waliopotea katika huduma na kujadili namna ya kuboresha zaidi huduma
katika vituo vya tiba na matunzo lakini pia kutoa elimu kuhusu haki za
WAVIU Washauri”,alieleza Tesha.
Naye
Mratibu wa Baraza la taifa la watu wanaoishi na VVU (NACOPHA), kanda ya
Mwanza, Veronica Joseph aliwasihi watu wanaoishi na maambukizi ya VVU
kujiweka wazi kwani itawasaidia kupata msaada kwa watu wanaowazunguka
ikiwemo familia zao.
“Wale
ambao hamjapima nawashauri mpime ili mjue afya zenu na ukibainika una
maambukizi ya VVU jiweke wazi ili usaidiwe,kujiweka wazi kutakusaidia
kuondoa matatizo na utaweza kupata fursa mbalimbali kutoka
wafadhili”,alileleza.
Katika
hatua nyingine alisema shirika la AGPAHI linatekeleza miradi ya Ukimwi
katika mikoa sita nchini ambayo ni Shinyanga, Simiyu, Geita,Mwanza,
Tanga na Mara kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania kwa ufadhili wa
serikali ya Watu wa Marekani kupitia Centres for Disease Control and
Preventation (CDC).
Mratibu
wa Masuala ya Watoto,Mama na Baba kutoka AGPAHI mkoa wa Shinyanga,
Aminael Tesha akizungumza wakati wa warsha ya siku tatu ya WAVIU
Washauri halmashauri sita za wilaya mkoa wa Shinyanga iliyofanyika
katika ukumbi wa Karena Hotel Mjini Shinyanga.
Aminael Tesha akielezea malengo ya warsha hiyo.
Mwezeshaji
katika warsha hiyo, Veronica Joseph ambaye ni Mratibu wa Baraza la
taifa la watu wanaoishi na VVU (NACOPHA), kanda ya Ziwa, akielezea
kuhusu umuhimu wa watu wanaoishi na maambukizi ya VVU kuwa wafuasi
wazuri wa dawa za kufubaza makali ya VVU na kujiweka wazi.
MVIU
Mshauri, Joyce Philimon kutoka mkoani Simiyu ambaye anaishi na
maambukizi ya VVU tangu mwaka 1997 akielezea umuhimu wa kujiweka wazi
pale unapobaini kuwa umepata maambukizi ya VVU. Kujiweka wazi kwa Joyce
kumfanya aishi salama na kwa amani na kupata fursa za kushiriki shughuli
mbalimbali kutoka kwa wadau.
MVIU
Mshauri Seleman Habibu kutoka Kahama akielezea namna alivyoweza kuishi
na maambukizi ya VVU tangu mwaka 2000 na ana watoto wawili ambao hawana
maambukizi ya VVU na mke wake pia hana maambukizi ya VVU.
Makamu
Mwenyekiti wa Baraza la Watu Wanaoishi na VVU katika Manispaa ya
Shinyanga,Vedastus Mutangira akizungumza katika warsha hiyo ambapo
akiwasisitiza watu wanaoishi na VVU kumeza dawa kwa utaratibu sahihi
uliowekwa pamoja na kuhudhuria kliniki mara kwa mara.
WAVIU Washauri wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yanajiri ukumbini.
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini.
Mwezeshaji
katika warsha hiyo,Vedastus Mutangira akitoa elimu kuhusu VVU na
Ukimwi. Aliwasisitiza watu wanaoishi na VVU kumeza dawa kwa utaratibu
sahihi uliowekwa pamoja na kuhudhuria kliniki mara kwa mara.
MVIU
Mshauri Neema Anthony kutoka kutoka CTC ya Segese katika halmashauri ya
wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga akichangia hoja wakati wa warsha
hiyo.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
0 comments:
Post a Comment