Home » » SHIRIKA LA AGPAHI LATOA SEMINA YA MATUMIZI YA FEDHA ZA WAFADHILI MJINI KAHAMA,WATUMISHI WABADHILIFU KUKIONA.

SHIRIKA LA AGPAHI LATOA SEMINA YA MATUMIZI YA FEDHA ZA WAFADHILI MJINI KAHAMA,WATUMISHI WABADHILIFU KUKIONA.



 MGANGA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA DR RASHID MFAUME AMBAYE ALIKUWA MGENI RASMI KATIKA SEMINA HIYO AKIWAMWAKILISHA KATIBU TAWALA WA MKOA WA GEITA NA SHINYANGA AKITOA NENO KWA WANA WARSHA.

KAHAMA

SERIKALI Imewaagiza watumishi  wa sekta ya Afya katika mkoa wa Shinyanga na Geita,kutumia  vizuri fedha za miradi ya ukimwi zinazotolewa na wafadhili ili ziweze kuwafikia walengwa na kuacha tabia ya kujinufaisha wenyewe kupitia fedha hizo.

Wito huo umetolewa leo na mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dr Rashid Mfaume kwa niaba ya makatibu tawala wa mkoa wa Shinyanga na Geita,wakati akifunga mafunzo ya siku mbili ya usimamizi wa fedha yaliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la AGPAHI.

Dr Mfaume amesema kumekuwa na tabia ya badhi ya watumishi wa Afya kutumia fedha za miradi ya wafadhili kwa kujinufaisha wenyewe huku walengwa wakikosa huduma muhimu ambazo zimekusudiwa kuwafikia.

Sambamba na hayo Dr Mfaume amewaagiza wakurugenzi wote wa halmashauri za mkoa wa Shinyanga na Geita kusimamia matumizi ya fedha za miradi ya ukimwi ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua watumishi watakaotumia vibaya fedha hizo.

Wakiongea kwa niaba ya wakurugenzi wa halmashauri za mkoa wa Shinyanga na Geita,Mkurugenzi wa Mbogwe Elias Kaendabila na mkurugenzi wa Halmashauri ya Shinyanga Ally Swedi wamelishikuru shirika la AGPAHI na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kupata huduma.

Kwa upande wake afisa Ruzuku mwandamizi wa Shirika la AGPAHI Leticia Gilba amesema kuwa,Shirika la AGPAHI Limetoa kiasi cha Shilingi Bilioni 36 kwa muda wa mwaka mmoja kwa mikoa sita ya Tanzania bara huku mkoa wa Shinyanga ukipata shilingi Bilioni 6.4 na Mkoa wa Geita Shilingi bilioni 4.2.

Akiitaja mikoa iliyopata fedha hizo Gilba amesema ni pamoja na Geita,Shinyanga,Mwanza,Tanga,Mara pamoja na mkoa wa Simiyu na kuongeza kuwa matarajio yao ni kuona fedha hizo zitatumika kama zilivyolengwa katika mikoa yote.

MATUKIO KATIKA PICHA:

WAJUMBE WA SEMINA HIYO KUTOKA HALMASHAURI ZA MKOA WA SHINYANGA NA GEITA WAKIWA KATIKA CHUMBA CHA MIKUTANO WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI MGENI RASMI HAYUPO PICHANI.
WATAALAMU WA SEKTA YA AFYA,WAHASIBU WAKIWA KATIKA SEMINA HIYO KATIKA HOTEL YA SUB MARINE ILIYOPO MJINI KAHAMA.

WAWAKISLISHI KUTOKA HALMASHAURI ZA SHINYANGA NA GEITA WAKIENDELEA NA SEMINA MJINI KAHAMA.
WAJUMBE WAKIWA MAKINI KUSIKILIZA KUHUSU UTUNZAJI WA MALI ZA HALMASHAURI ZINAZOTOLEWA NA SHIRIKA LA AGPAHI.

KUSHOTO NI MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MBOGWE MKOANI GEITA ELIUS KAYANDABILA AKIWA NA WAJUMBE WENGINE KATIKA SIKU YA PILI YA SEMINA HIYO.

WAJUMBE WAKIWA KATIKA SEMINA ILIYOANDALIWA NA SHIRIKA LA AGPAHI ILIYOFANYIKA KATIKA HOTEL YA SUB MARINE MJINI KAHAMA.

AFISA RUZUKU KUTOKA SHIRIKA LA AGPAHI ALFRED MDEE AKITOA ELIMU KUHUSU MATUNZO YA VIFAA VYA HALMASHAUI VINAVYOTOLEWA NA SHIRIKA LA AGPAHI.

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MBOGWE MKOANI GEITA ELIUS KAYANDABILA AKITOA UFAFANUZI NAMNA AMBAVYO HALMASHAURI YAKE INAVYOSIMAMIA UTEKELEZAJI WA NA USIMAMIZI WA FEDHA ZA MIRADI YA UKIMWI.

AFISA RUZUKU WA SHIRIKA LA AGPAHI JOHN NNKO AKITOA SEMINA MBELE WA WAJUMBE KATIKA SEMINA HIYO.

WAJUMBE WAKICHANGAMSHA MWILI BAADA YA KUKAA KWA MUDA MREFU.

DR JAPHET SIMEO MGANGA MKUU WA MKOA WA GEITA AMBAYE ALIKUWA MWENYEKITI WA SEMINA HIYO AKITOA UFAFANUZI WA JAMBO KATIKA SIKU YA PILI YA SEMINA HIYO.

AFISA MRADI MWANDAMIZI WA SHIRIKA LA AGPAHI JULIUS SIPEMBA AKITOA NENO LA SHUKRANI KWA WAJUMBE WALIOHUDHURIA KATIKA KIKAO HICHO.

DR SHANI JOSEPHAT  KUTOKA KISHAPU AKIULIZA SWALI KATIKA SEMINA HIYO

ZAINAB RUSATRA KUTOKA HOSPITALI YA MKOA WA GEITA AKIULIZA SWALI KATIKA HIYO.

MJUMBE KUTOKA HALMASHAURI YA MBOGWE AKIULIZA SWALI KATIKA SEMINA HIYO.
MJUMBE KUTOKA USHETU AKIULIZA SWALI KATIKA SEMINA HIYO


AFISA RUZUKU MWANDAMIZI WA SHIRIKA LA AGPAHI LETICIA GILBA AKIFAFANUA JAMBO KATIKA SEMINA HIYO LEO.


DR JAPHET SIMEO MGANGA MKUU WA MKOA WA GEITA AMBAYE ALIKUWA MWENYEKITI WA SEMINA HIYO AKITOA SHUKRANI BAADA YA KUFUNGA SEMINA SIKU YA PILI.
WAJUMBE WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA BAADA YA KUMALIZA SIKU YA PILI YA SEMINA MJINI KAHAMA.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa