Naibu
Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akihutubia mamia ya wachimbaji
wadogo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha
Mwazimba, Kata ya Chela, Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, Jana 3
Februari 2018. Picha zote Na Mathias Canal
Naibu
Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua maeneo ya uchimbaji
baada ya mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mwazimba, Kata
ya Chela, Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, Jana 3 Februari 2018
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua maeneo ya wachimbaji wadogo wa chama cha ushirika cha Kasi Mpya Gold Mine katika Kijiji cha Mwazimba, Kata ya Chela, Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, Jana 3 Februari 2018
Naibu
Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akihutubia mamia ya wachimbaji
wadogo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha
Mwazimba, Kata ya Chela, Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, Jana 3
Februari 2018.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua maeneo ya wachimbaji wadogo wa chama cha ushirika cha Kasi Mpya Gold Mine katika Kijiji cha Mwazimba, Kata ya Chela, Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, Jana 3 Februari 2018
Na Mathias Canal, Shinyanga
Naibu
Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ametatua mgogoro wa leseni
uliodumu kwa takribani miaka kumi kwa kuamuru kupitia haraka eneo la
leseni ya uchimbaji wa madini kwa wachimbaji wadogo wa chama cha
ushirika cha Kasi Mpya Gold Mine.
Mhe
Biteko ametoa agizo hilo Jana 3 Februari 2018 wakati akihutubia mamia
ya wachimbaji wadogo waliohudhuria kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
katika Kijiji cha Mwazimba, Kata ya Chela, Wilayani Kahama kufuatia
malalamiko ya Mbunge wa Jimbo la Msalala Mhe Ezekiel Maige sambamba na
malalamiko ya wachimbaji wadogo waliyoyawasilisha Wizara ya Madini Mjini
Dodoma Januari 26, 2018.
Alisema
kuwa wananchi walifunga safari mpaka ofisi za madini kwa ajili ya
kupata uhalali wa kupimiwa eneo lao kwa kutumia GPS lakini Kaimu Afisa
madini mkazi Wilaya ya Kahama akawabadilishia Nukta (Coordinator) ambazo
baadaye zilionekana kuwa za eneo jingine ambalo ni mbuga isiyokuwa na
madini huku eneo hilo likihamishiwa kwa ntu mwingine.
Mhe
Biteko amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya madini Prof Simion Msanjila
kumchukulia hatua za haraka za kinidhamu aliyekuwa Kaimu Afisa madini
mkazi Wilaya ya Kahama aliyehusika na upotoshaji wa leseni na kuzua
mgogoro wa usumbufu usiokuwa na sababu dhidi ya wananchi na serikali.
Alisema
kuwa hakuna sababu ya Wizara ya Madini kukumbatia mgogoro huo wa leseni
uliodumu kwa miaka kumi kwa sababu ya eneo ambalo lilipotoshwa na
baadhi ya watendaji wa Wizara ya madini kwani jukumu la serikali ni
kuwatumikia wananchi ikiwemo utatuzi wa kadhia mbalimbali zinazowakabili
katika jamii.
Mhe
Biteko kwa msisitizo mkubwa amewataka wachimbaji wadogo kuwa waaminifu
na kufichua baadhi ya wachimbaji wanaoficha madini kwa kutorosha bila
kulipa kodi kwani kufanya hivyo itakuwa njia pekee ya kuisaidia serikali
na kuinusuru katika mtego wa wizi wa rasilimali hizo.
Ameongeza
kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli haitawafumbia macho
wamiliki wa leseni hizo ambao leseni zao zimedumu kwa muda mrefu bila
kuzifanyia kazi kwani hawazalishi ajira yoyote wala kulipa kodi Hivyo
serikali imekusudia kuzifuta na kuwapa watu wengine ambao watazifanyia
kazi haraka iwezekanavyo ili kuongeza tija kwa sekta ya madini katika
uchangiaji wa pato la Taifa.
Akitoa
mfano katika eneo la Kahama kuna leseni 249 lakini zinazofanyiwa kazi
ni 18 tu huku wenye leseni zisizofanya kazi wakisubiri wachimbaji wadogo
wavumbue madini kisha huja kuwaondoa kwa kisingizio cha umiliki wa
leseni. Leseni hizo zikiwa zimedumu kwa muda mrefu bila kuendelezwa.
Aidha,
alisema kuwa kuna maeneo makubwa manne ambayo yameshaamuliwa na
serikali kutengwa kwa ajili ya wachimbaji wadogo ikiwemo eneo la
Nyang'wale lenye hekari 996, eneo la Nyangarata lenye hekari 1074, Eneo
la Buzwagi kilometa za mraba 53.4 na eneo la Kinamyuba kilomita za mraba
33.3
Alisema
kuwa jukumu la serikali ni kutatua kero za wananchi sio kuwaongezea
kero wananchi hivyo watendaji wote wa serikali wanapaswa kutimiza ndoto
ya Rais Magufuli kwa kuwatumikia wananchi kwa imani na matendo imara kwa
kuwanufaisha watumishi na rasilimali zao.
Sambamba
na hayo Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko amewataka
wananchi kuendelea na uchimbaji wakati taratibu zikifuatwa kukamilisha
kumaliza mgogoro huo huku akiwahakikishia kutoondolewa tena na endapo
kama watakuwa wanahitaji maeneo mengine yaliyotengwa kwa ajili ya
wachimbaji wadogo wanapaswa kufuata taratibu za kisheria zilizoainishwa.
Awali
mbunge wa Msalala Mhe. Ezekiel Maige alimweleza Mhe. Naibu Waziri kuwa
watu wake wameonewa kwa muda mrefu na yeye akifuatilia mgogoro huo bila
mafanikio.
"Ni
kwasababu ya serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Magufuli
kwa kimbilio la wanyonge, mheshimiwa Naibu Waziri nilikua nimekata
tamaa" Alikaririwa Mhe Maige aliyekuwa akizungumza kwa hisia huku
akishangiliwa na mamia ya wachimbaji wadogo waliokisanyika kwenye
mkutano huo.
0 comments:
Post a Comment