Home » » SHY KUWASAKA WALIOFANYA UDANGANYIFU KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA

SHY KUWASAKA WALIOFANYA UDANGANYIFU KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA


Mwandishi wetu, Kahama
SERIKALI wilayani Kahama imeanza msako kwenye Shule za sekondari za Kata wa kuwasaka wanafunzi ambao hawana sifa waliojiunga na masomo kwa kutumia njia za udanganyifu ikiwemo kugushi majina yasiyokuwa yao.
Afisa Elimu wa Sekondari wilayani Kahama,Gwasa Joseph amesema msako huo umeanza kwa kupita kila shule kubaini wanafunzi hao ambao mwishoni mwa wiki iliyopita wanafunzi zaidi ya mia mbili walibainika katika vidato vya pili na nne.
Hata hivyo idadi hiyo  inaweza kuongezeka kutokana na zoezi hilo kubaini wanafunzi hao katika shule moja tu kati ya 46 za Serikali zilizopo wilayani Kahama ambazo zinadaiwa kuwa ndio vinara vya wanafunzi wasiokuwa na sifa za kuingia sekondari kuwaingiza.
 
Imedaiwa kuwa wanafunzi hao kwa kushirikiana na walimu wasiokuwa waaminifu wamekuwa wakiingizwa shuleni kwa kutumia majina ya wanafunzi walioshindwa kuripoti kwemnye shule hizo za Sekondari za Kata ambao hupelekwa na wazazi wao kwenye shule zingine.
 
 
Hali hiyo imetokana na  wazazi  kuwahamishia shule zingine watoto wao waliofaulu kujiunga na shule za kata hali ambayo hutoa nafasi ya walimu kuingiza wanafunzi wasiokuwa na sifa tatizo ambalo wilayani Kahama ni kubwa ambalo ndio chanzo cha kushuka kwa kiwango cha elimu mkoani Shinyanga.
 Blogzamikoa      

0 comments:

 
Supported by Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa