Home » » CHADEMA WAWASHUSHIA KIPIGO WANACHAMA WA CCM KAHAMA

CHADEMA WAWASHUSHIA KIPIGO WANACHAMA WA CCM KAHAMA

WATU sita wafuasi wa Chama cha Mapinduzi CCM wilayani Kahama wamejeruhiwa vibaya baada ya kucharangwa mapanga kwenye kampeni za Uchaguzi mdogo wa Udiwani Kata ya Ubagwe katika Halmashauri ya Ushetu.

Katika vurugu hizo yumo pia Afisa Mtendaji wa kata hiyo Alphonce Kimaro ambaye amejeruhiwa vibaya kwa kukatwa mapanga kichwani.

Muuguzi Mkuu katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama;Richard Mabagala amewataja wengine waliojeruhiwa kwa mapanga na kulazwa hospitalini hapo ni pamoja na Sebastian Masunga {34].

Aidha Mabagala amewataja wengine ni pamoja na Ramadhani Salumu,Subira Nyangusu  na Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Kahama;Masuod Melimeli{34} pamoja na dreva wa gari la CCM wilaya;Charles Peter {55} .

Hata hivyo Mganga Mkuu wa wilaya ya Kahama;Andrew Emanuel amesema Kimaro,Masunga na Peter hali zao ni mbaya wamepelekwa hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza.

Kwa mujibu wa Habari za polisi zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga;Evarist Mangala tayari watuhumiwa 16 wa tukio hilo wamekamatwa akiwemo Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki, Sylvester Kasulumbayi wote wakiwa wafuasi wa  Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.

0 comments:

 
Supported by Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa