Home » » Compassion yasomesha watoto 70,000

Compassion yasomesha watoto 70,000

Mchungaji Joseph Mitinje, Mkurugenzi wa CompassionSHIRIKA la kimataifa la Compassion linalofanya kazi na madhehebu ya Kikristo nchini, limefadhili wanafunzi 70,000 wanaosoma shule na vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Akizungumzia ufadhili huo jana alipokutana na waamini wa makanisa ya Kiinjili mjini hapa, Mkurugenzi wa shirika hilo nchini, Mchungaji Joseph Mitinje, alisema kazi wanazofanya zimefanikiwa katika elimu.
Mchungaji huyo aliongeza kwamba katika kipindi cha miaka 15 tangu kuanzishwa kwa shirika hilo Wilaya ya Kahama imesomesha watoto 1,000 na vituo sita vya kuhudumia, ambavyo vimefadhiliwa na Compassion.
Kwa mujibu wa Mchungaji Mitinje, shirika hilo lipo kwenye nchi 28 duniani kote huku mwasisi wake ni Korea Kusini, ambako mpango wa kusaidia watoto ulianzia.
Alisema katika Afrika Mashariki ukiondoa Tanzania shirika hilo lipo Rwanda, Kenya, Uganda na Ethiopia na tayari limezalisha wasomi wengi wakiwemo madaktari na wauguzi.
Kabla ya hapo Mwenyekiti wa wachungaji kutoka makanisa sita washirika wa shirika hilo la Compassion, Mchungaji Felix Gwamuye, aliomba idadi ya watoto wanaosomeshwa iongezeke
Chanzo;TanzniaDaima

0 comments:

 
Supported by Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa