Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Madiwani
wa wili wa chama cha chadema katika manspaa ya Shinyanga wameachia nafasi zao
kwa madai ya kukosa imani na uongozi wa juu wa chama hicho kwa kuendekeza
migogoro na kuwaita baadhi ya wanachama wasaliti.
Madiwani
waliongatuka katika chama hicho ni Sebastian Peter diwani wa kata ya Ngokolo na
Zacharia mfuko kata ya Masekolo ambao wamekabidhi barua zao kwa mkurugenzi wa
manspaa ya Shinyanga.
Awali
wakiongea na waandishi wa habari madiwani hao wanasema uongozi wa
juu wa chama hicho umekuwa ukiendekeza migogoro ndani ya chama pamoja na
ubinafisi pia ahadi zao zimekuwa sio za kweli za kumjengea nyumba mjana wa
aliyekuwa mgombea ubunge marehemu Shilembi magadula.
Aidha
madiwani hao wamesema migogoro hiyo itasababisha kukisambaratisha chama hichi
kwani viongozi wa juu akiwemo katibu mkuu na mwenyekiti wamekuwa na ubaguzi wa
ukabira
Katibu
wa chama cha chadema mkoa wa Shinyanga Nyangaki Shilungu Shella amesema chama
chake kimepata pigi lakini watajipanga vyema kuhakikisha kata hizo
wanazichukuwa wakati wa uchaguzi mdogo.
Chadema
walikuwa na madiwani 8 baada ya 2 kuachia ngazi wamebaki 6 wakati ccm wakiwa na
madiwani 17 katika baraza la madiwani.
0 comments:
Post a Comment