Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Lumato anasema hata eneo likionyesha dalili nzuri za awali kama ilivyo
katika Bonde la Ruhuhu ni lazima sehemu hiyo ichimbwe na matokeo
yaonyeshe kiasi cha rasilimali kinachoweza kuzalishwa kibiashara
Makala hii inamsaidia mwajiri na mwajiriwa kujua jinsi ya
kupeana na kuomba likizo kwa mujibu wa sheria ya ajira na mahusiano
kazini na. 6 ya mwaka 2004. Sheria hii inatoa muongozo jinsi ya kupeana
likizo na aina ya likizo ambazo muajiriwa anapaswa kupewa.
Likizo zote anayepaswa kupewa ni yule aliyefanya
kazi zaidi ya miezi sita mfululizo, au kama alifanya akatoka halafu
akafanya tena basi hizo siku zisizidi miezi sita atakuwa na haki ya
kupata likizo. Tunapoongelea likizo tuna maana likizo yenye malipo, siyo
unampa mtu likizo lakini mshahara haumpi hicho ni kinyume cha sheria.
Likizo ya mwaka (Annual Leave) hii ni likizo ya
siku 28 ambayo kila mfanyakazi anapaswa kuipata kila mwaka, haijalishi
mfanyakazi huyu yuko sekta gani iwe mlinzi, dereva au mfanyakazi wa
ndani.
Hii likizo inapaswa kutolewa na mwajiri na endapo
mtakubaliana kuwa badala ya kwenda likizo mfanyakazi huyu anapaswa
kuendelea kufanyakazi basi mshahara wa mwezi mmoja alipwe huyu
mfanyakazi kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano
Kazini ya mwaka 2004.
Likizo ya ugonjwa (Sick Leave), hii ni likizo
inayotolewa kwa mgonjwa ambaye ni mwajiriwa na ana haki ya kupata likizo
hii ya ugonjwa ambayo ni siku 126, siku 63 ni mshahara wote na siku 63
zinazofuata nusu mshahara, pia mtu huyu hawezi kupewa likizo hii endapo
atashindwa kutoa uthibitisho wa daktari au endapo anapewa mafao kutoka
kwenye makubaliano ya pamoja au kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.
Likizo ya kifo (Compassionate Leave), hii ni
likizo kwa mfiwa, endapo mfanyakazi atafiwa na mtu wake wa karibu, baba,
mama, dada, mke au mtoto ana haki ya kupata likizo ya siku nne. Pia
likizo hii inaruhusiwa endapo mfanyakazi anauguliwa na mtoto mdogo.
Hii ni haki ya mfanyakazi endapo atathibitisha
uwepo wa hilo tukio tajwa, hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 34 cha
Sheria ya Ajira ya mwaka 2004.
Likizo ya Uzazi kwa mwanamke (Maternity Leave) ni
likizo maalumu ya siku 84 na endapo atajifungua watoto mapacha basi
anapata likizo ya siku 100, pia huyu mwajiriwa anapaswa kupewa muda wa
saa mbili wa kazi kwa ajili ya kumnyonyesha mtoto, endapo mtoto
atafariki ndani ya mwaka mmoja anapaswa kupewa likizo ya uzazi endapo
atashika mimba.
Taarifa ya likizo itolewe kwa mwajiri ndani ya
miezi mitatu juu ya lini likizo inachukuliwa. Pia mama anayenyonyesha
haruhusiwi kufanya kazi zinazohatarisha afya yake na ya mtoto, mjamzito
anaweza kuchukua wakati wowote wiki nne kabla ya kujifungua na
inawezakuwa mapema zaidi endapo daktari atathibitisha hilo.
Likizo ya uzazi kwa mwanaume (Paternity Leave) hii ni likizo maalumu kwa wanaume ambao wake zao wamejifungua.
Ni likizo ya siku tatu na inapaswa kuchukulia
ndani ya siku saba toka mke kajifungua, unachopaswa ni kumtaarifu
mwajiri na kuthibitisha kuwa aliyejifungua ni mkeo, hii ni kwa mujibu wa
kifungu cha 34 (1) a cha sheria ya ajira ya mwaka 2004. Kimsingi ni
suala la msingi sana kwa wafanyakazi kuzijua haki zao.
Makala hii itaendelea alhamisi ijayo, waambie
waajiriwa wengine waisome ili waweze kujua haki zao ambazo nyingi
zinamezwa na baadhi ya waajiri nchini
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment