Afisa
Ardhi na Mazingira wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala (Kahama), Zablon
Donge, akifungua rasmi warsha ya siku tatu ya wadau wa mapambano dhidi
ya UKIMWI kwa niaba ya Mkurugenzi wa wilaya hiyo, iliyofanyika Kata ya
Segese wilayani Kahama mkoani Shinyanga. Kushoto kwake ni Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues pamoja na Afisa Mradi wa
Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias.
Na Mwandishi Wetu, Kahama
MKURUGENZI
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues ametaka jamii
kujumuisha suala la utamaduni katika kupambana na maambukizi mapya ya
Ukimwi.
Alisema
hayo kwenye warsha ya siku tatu ya wadau wa mapambano dhidi ya UKIMWI
inayofanyika Kata ya Segese wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Alisema
katika ufunguzi huo kwamba kwa miaka mingi pamoja na kuwepo kwa elimu
ya UKIMWI, kumekosekana mabadiliko yanayotakiwa kukabili maambukizi
mapya.
Alisema
UNESCO iliangalia tatizo hili na kubaini kwamba kutobadilika kwa hali
kumetokana na kutounganishwa kwa kipengele cha mila ambacho ndicho
kinachofanya kuwepo na mazingira rafiki ya kupashana habari.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akizungumza na
washiriki wakati wa uzinduzi wa program ya utamaduni kukabili UKIMWI
itakayoendeshwa na shirika lake.
Warsha
hiyo ya Siku tatu imelenga katika kuhamasisha jamii, Shule, Asasi,
Taasii za Dini na Serikali katika utoaji wa Elimu sahihi ya huduma
rafiki za Afya ya Uzazi, VVU/UKIMWI, ujinsia na maadili ya Afya kwa
vijana balehe na vijana.
Amesema
mpaka sasa utoaji wa elimu ya afya, ueleweshaji wa ugonjwa haujafanya
mabadilikoya kutosha kutokana na ukweli kuwa katika utekelezaji wa
kampeni masuala ya utamaduni na uwasilishaji wa taarifa haukuwa
umezingatiwa.
Alisema
wakati Kahama (Msalala) kwa sasa kiwango cha maambukizi ni asilimia
5.9, Juhudi zinatakiwa kufanywa katika kuhakikisha kwamba elimu
inayotolewa inahusishwa na masuala ya kitamaduni ili kubadilisha maisha
ya wakazi.
Alisema katika mapambano ya maambukizi mapya mila na utamaduni zinaweza kabisa kusaidia kukabiliana na maambukizi ya UKIMWI.
Afisa
Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias
akielezea madhumuni ya warsha hiyo ya siku tatu iliyojumuisha makundi
mbalimbali ikiwemo Waganga wa jadi, wakunga wa jadi, viongozi wa dini,
viongozi wa vijiji na kata, walimu, wataalamu wa afya na elimu na Asasi
zisizokuwa za kiserikali.
Alisema
program inayoangaliwa sasa ni ile iliyoleta mafanikio katika nchi
kadhaa za Afrika ikiwamo Msumbiji na hivyo wanaona waijaribu Tanzania
katika wilaya sita ikiwemo Kahama na hasa halmashauri ya wilaya ya
Msalala.
Alisema
pamoja na watu wengi kutibiwa na waganga wa kienyeji ni vyema
watengeneza sera na watu wengine kutambua umuhimu wao ili kwa kupitia
mila waweze kuwafunua watu akili na kujikinga na maambukizi ya UKIMWI.
Alisema
anaamini kuwa mila na tamaduni zikitumika vyema na hata matibabu
zitasaidia kuokoa maisha ya wengi na pia kuzuia maambukizi mapya.
Alisema
maambukizi mapya ni tatizo kwa sasa hasa ikizingatiwa kwamba wananchi
wengi wanajua uwapo wa UKIMWI lakini ufahamu ni mdogo kwa kuwa katika
kufundisha watu hawakupewa elimu ya kutosha inayoambatana na kuangalia
mila na desturi njema za afya zilizopo.
Afisa
afya mkuu kitengo cha elimu ya afya kwa umma-programu ya afya mashuleni
kutoka Wizara ya afya na ustawi wa jamii, Avit Maro akielezea jambo kwa
washiriki kuhusiana na masuala ya afya ya uzazi wakati wa warsha ya
siku tatu ya wadau wa mapambano dhidi ya UKIMWI iliyofanyika Kata ya
Segese wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Alisema ni vyema wananchi wakatumia mali asili waliyonayo kufundishana juu ya kukabiliana na maambukizi mapya ya UKIMWI.
Alisema
UNESCO imeamua kuanzisha programu maalumu ya kutumia mila na desturi
kukabili UKIMWI kama njia nyingine ya kuoanisha nguvu katika mapambano
dhidi ya maambukizi mapya.
Naye
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala (Kahama),
Zablon Donge alishukuru UNESCO kwa kuanzisha program ya kujifunza namna
ya kukabiliana na maambukizi mapya ya UKIMWI.
Alisema
ukiwa na halmashauri ya wagonjwa huwezi kuwa na halmashauri kwa kuwa
shughuli za kiuchumi na kijamii kushindikana kutekelezwa, na kusema kuja
kwa UNESCO ni msaada mkubwa.
Warsha
hiyo imejumisha makundi mbalimbali ikiwemo Waganga wa jadi, wakunga wa
jadi, viongozi wa dini, viongozi wa vijiji na kata, walimu, wataalamu wa
afya na elimu na Asasi zisizokuwa za kiserikali.
Mkurugenzi
msaidizi masuala mtambuka kutoka Wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi,
Dkt. Laetitia Sayi akifafanua jambo jinsi wizara yake inavyoshirikisha
jamii katika utoaji wa elimu mashuleni hususani afya ya uzazi,
VVU/UKIMWI huku ikishirikiana na wadau wao wa karibu UNESCO.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues, akiendesha warsha
hiyo kwa njia ya majadiliano na washiriki juu ya dhana na maana ya
balehe, vijana balehe na vijana sambamba na maana ya mimba na ndoa za
utotoni.
Pichani
juu na chini ni sehemu ya washiriki hao wakifuatilia majadiliano kwenye
warsha hiyo ya siku tatu iliyofanyika Kata ya Segese wilayani Kahama
mkoani Shinyanga.
Pichani
juu na chini ni baadhi ya washiriki wakichangia maoni wakati
majadiliano ya kutafuta suluhu ya kupunguza maambukizi mapya ya
VVU/UKIMWI, mimba na ndoa za utotoni kwenye jamii zao.
Sehemu
ya washiriki warsha hiyo kwenye vikundi kazi wakianisha na kubainisha
matatizo yanayowakabili vijana balehe na vijana katika jamii zao huku
wakiongozwa na Mkurugenzi msaidizi masuala mtambuka kutoka Wizara ya
elimu na mafunzo ya ufundi, Dkt Laetitia Sayi (kushoto).
Mshiriki akiwasilisha kazi za vikundi baada ya majadiliano.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akifafanua baadhi ya
changamoto zilizoanishwa kwenye vikundi kazi na washiriki wakati wa
warsha hiyo ya siku tatu.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment