Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Kadama
 Malunde Mwenyekiti Mpya wa Wanahabari Shinyanga
Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
CHAMA cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press 
Club-SPC) jana Julai 23, 2015 kimefanya Uchaguzi wake Mkuu wa viongozi 
watakaokiongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo 
ambapo mwanahabari, Kadama Malunde amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa 
chama hicho.
Akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa Uchaguzi huo Mkuu wa SPC 
uliofanyika mjini Shinyanga, David Nkulila alisema, Malunde ametwaa 
nafasi hiyo baada ya kuwashinda wagombea wenzake watatu ambao ni Patrick
 Mabula, Marco Mipawa na Greyson Kakuru.
Kadama Malunde ni mwandishi wa habari wa gazeti la Mtanzania, Kahama FM 
na Mkurugenzi wa Malunde1 blog ambayo ni blogu Mwanachama wa Chama cha 
Blogu Tanzania (Tanzania Bloggers Network, TBN).
Nkulila aliwataja viongozi wengine wapya waliochaguliwa kuwa ni Stephen 
Wang’anyi akichaguliwa kuwa Katibu Mkuu, Shaaban Alei kuwa Makamu 
Mwenyekiti, Katibu Msaidizi Ally Lytawi na mweka hazina ni Stella 
Ibengwe pamoja na kamati tendaji ya wajumbe watano.
Baada ya kutangaza matokeo hayo Nkulila amewataka wanachama wa klabu 
hiyo, kuachana na tofauti zillizokuwepo wakati wa uchaguzi na badala 
yake kushirikiana na viongozi waliowachaguliwa ili kuleta maendeleo na 
mabadiliko katika klabu hiyo.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi, Mwenyekiti mpya wa SPC, 
Kadama aliwashukuru wanachama wote wa chama hicho kwa kumkubali aweze 
kushirikiana nao kuweza kutatua changamoto mbalimbali za wanahabari 
mkoani hapo pamoja na kuleta maendeleo kwa klabu hiyo. Aidha aliahidi 
kutenda haki kwa kila mmoja na kuzingatia katiba ya chama katika 
utendaji wa kazi za chama.
Kwa upande wake Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Felician amewataka 
viongozi wapya wa klabu hiyo kuendeleza misingi ya ushirikiano 
waliouacha na kuwasisitiza kufanya kazi kwa uwazi na ukweli huku 
wakizingatia maadili ya wanahabari.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment