Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi,Mhandisi Philbert
Rweyemamu(kushoto) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Bi Josephine
Matiro wakati wa uzinduzuzi wa jengo la Maabara katika shule ya
Sekondari Ngokolo lililojengwa kwa ufadhili wa kampuni ya kuchimba
Dhahabu ya Buzwagi.
Jengo la Maabara
lililojengwa kwa ufadhili wa Mgodi wa Kuchimba Dhahabu wa Buzwagi
katika shule ya sekondari Ngokolo iliyopo wilani Shinyanga.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi,Mhandisi Philbert Rweyemamu akizungumza na waandishi wahabari mara baada ya kukabidhi majengo ya Maabara hizo.
Baadhi ya wananchi katika Manispaa ya Shinyanga waliojitokeza kushuhudia makabidhiano ya Maabara hizo.
Mkuu
wa wilaya Shinyanga Bi Josephine Matiro akisisitiza jambo wakati
alipokuwa akizungumza na baadhi ya wananchi waliojitokeza kushuhudia
kukabidhiwa kwa maabara hizo ambazo zimejengwa kwa msaada wa Kampuni ya
Kuchimba Dhahabu ya Acacia kupitia Mgodi wa Buzwagi.
Naibu
waziri ofisi ya makamu wa Rais na Mbunge wa Shinyanga Mjini Mh. Steven
Masele akitoa maneno ya shukurani kwa kampuni ya kuchimba Dhahabu ya
Acacia kwa msaada wa ujenzi wa maabara kwa baadhi ya shule za sekondari
katika manispaa ya Shinyanga.
Meneja
Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Philbert Rweyemamu akimkabidhi Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Bi Josephine Matiro jengo la maabara la shule ya Sekondari ya Mazinge ambalo limejengwa kwa ufadhili wa kampuni yaKuchimbaDhahabu ya Acacia. Anayepiga makofi ni mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Mh Steven Masele.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini aliyekuwa mkoani Shinyanga.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini aliyekuwa mkoani Shinyanga.
Kampuni
ya Uchimbaji wa Madini ya Acacia kupitia mgodi wake wa Buzwagi imetumia
zaidi ya shilingi Mil 400 kukamilisha miradi minne ya ujenzi wa vyumba
vya maabara katika Shule za sekondari za Mazinge, Kizumbi, Ngokolo na
Old Shinyanga zote za Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi maabara hizo, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi
Mhandisi Philbert Rweyemamu amesema, Acacia imekuwa ikitekeleza miradi
mbalimbali ya maendeleo yote ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya
kampuni ya kufanya uchimbaji unaojali na hususani kwa kutekeleza miradi
katika maeneo yanayozunguka migodi ya Acacia.
Kukamilika
kwa miradi hii kunatajwa kuwa kutasaidia katika kukabiliana na
changamoto ya upatikanaji wa wataalamu wa sayansi katika maeneo
mbalimbali hapa nchini “Matumaini ya Kampuni ya Acacia ni kuona Tanzania
inapata wataalamu wengi katika fani za Sayansi, ambao watasaidia katika
maendeleo ya taaluma hii” Alisema Injinia Philbert Rweyemamu.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mjini Bi Josephine Matiro
ameupongeza Mgodi wa Buzwagi kwa namna ambavyo umekuwa ukishirikiana na
wananchi wa Shinyanga katika kukamilisha miradi mbalimbali. “ Wananchi
wetu wengi ni wa kipato cha chini, msaada huu mlioutoa ni mkombozi kwao
lakini pia kwa watoto wetu maana mmetutengenezea mazingira mazuri ya
watoto wetu kusoma na hapana shaka hawa watabadili hali ya maisha yetu
na kuwa mazuri pindi watakapohitimu masomo yao” Alisema Mkuu huyo wa
Wilaya.
0 comments:
Post a Comment