Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Halmashauri ya Mji wa Kahama Mkoani Shinyanga imewasimamisha
kazi watumishi wake watano na wengine watano kuwaweka kwenye uchunguzi maalumu
baada ya kubainika na ubatilifu wa fedha shilingi milioni mia nane arobaini na
tatu zilizotolewa ushuru wa huduma na mgodi wa Buzwagi uliopo Wilayani Kahama.
Uamuzi wa kuwasimamisha watumishi hao umetangazwa leo na
mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Abel Shija baada ya kumalizika jana kwa kikao
cha baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo ambao walilidhia kusimamishwa kazi
kwa watumishi hao.
Shija amewataja watumishi waliosimamisha ni pamoja na Michael
Nzingula ambaye ni mkuu wa idara ya kilimo, ushirika na umwangiliaji
pamoja na afisa ugavi katika Halmashauri hiyo Joseph Maziku na afisa biashara
Elius Mollel pamoja na mweka hazina katika Halmashauri hiyo Wilfredy Kisheri na
mhasibu wake Alex Mloso.
Watumishi hao walikuwa wajumbe wa bodi ya zabuni ambao kwa
pamoja wanatuhumiwa kutoa zabuni za ujenzi kwenye makampuni yaliyofutwa na
msajili zenye thamani ya shilingi bilioni moja na milioni mia sita, milioni
moja na nusu kati ya hizo zimetolewa ushuru wa huduma na mgodi wa Buzwagi.
Hata hivyo Shija amesema katika ubatilifu huo shilingi milioni
mia nane thelathini kati ya fedha hizo hazijulikani matumizi yake na
katika watumishi hao wengine watano wako kwenye uchunguzi ambao walikuwa
wajumbe wa bodi hiyo iliyohusika kufanya ubatilifu wa fedha hizo.
Mwenyekiti huyo amewataja watumishi ambao wako kwenye uchunguzi
zidi ya tuhuma hizo ni pamoja na Afisa utumishi mkuu wa Halmashauri hiyo Kulwa
Ntaudyimara, Afisa elimu wa sekondari Anastazia Manumbu, Afisa ardhi mipango
mji Joakim Henjewele, afisa elimu msaidizi Neema Lema pamoja na afisa mipango
Angela Cravery.
Pia katika tuhuma hizo yumo aliyekuwa mkurugenzi katika
Halmashauri hiyo Felix Kimalio aliyehamishiwa Wilaya ya Longido na mhandisi
wake Msumba Msoka aliyehamishiwa Wilaya ya Nanyumbu ambao taratibu za
kiutumishi za kurejeshwa Kahama kujibu tuhuma zao zinafanyika huku Jodan Ojode
aliyekuwa afisa mipango kabla ya kuhamishwa akiibuka kidedea baada ya
kukataliwa kwa ushauri wake wa kutotumia vibaya fedha hizo.
Kabla ya hapo mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kawawa aliunda
kamati ya uchunguzi wa matumizi ya fedha hizo ambapo alibaini kuwepo kwa
ubatilifu wa fedha hizo hali ambayo aliiangiza baraza la madiwani kuchukua hatua
kali za kisheria na nidhamu dhidi ya wahusika wote waliohusika kutumia vibaya
fedha hizo.
0 comments:
Post a Comment