MKURUGENZI wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Kiomoni Kibamba,
amesema halmashauri hiyo ina deni la Sh bil 22, zikiwemo za miongoni
mwake ikiwa ni ya madiwani waliopita waliokopwa katika utekelezaji wa
vikao mbalimbali.
Hayo aliyasema juzi mbele ya Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela.
Alisema pia uwezo wa kujiendesha halmashauri ni asilimia 2.09 hivyo
bila fedha za serikali kuu halmashauri ingekuwa kwenye hali mbaya.
Kibamba katika mchanganuo wa taarifa yake ya bajeti ya fedha na
uendeshaji alisema kati ya Sh bil 22, madiwani wanadai Sh mil 43.3 na Sh
mil 10 kwa anayetoa huduma za vifaa vya ofisi pamoja, ikiwemo kompyuta.
Pia alisema kumekuwepo na changamoto ya ukamilishaji wa majengo
yaliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi, ikiwemo ukamilishaji wa kituo cha
Polisi kilichopo kata ya Didia kilichotengewa bajeti yake ya Sh milioni
tano.
Mongela aliwataka madiwani kuwa wabunifu wa vyanzo vya mapato na
kuweka fedha za akiba katika uendeshaji bila kubadili matumizi
yaliyokusudiwa.
CHANZO GAZETI LA HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment