Mkuu
wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Kijuu (wa nne kushoto) na Mkuu wa
mkoa wa Shinyanga Bi. Zainabu Telack (wa pili kulia) wakielekea eneo la kupokea
misaada iliyotolewa na wananchi wa Shinyanga.
(Picha/Habari
na Eleuteri Mangi, Bukoba)
Mkoa
wa Shinyanga umekabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi na chakula vyenye thamani ya
Sh. milioni 41,172 kwa uongozi wa mkoa wa Kagera ili kusaidia waathirika wa
tetemeko la ardhi lililotokea mkaoani humo hivi karibuni.
Makabidhiano
hayo yalifanywa leo mjini Bukoba kati ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi. Zainabu
Telack ambaye aliambatana na baadhi ya viongozi wa mkoa na viongozi wa dini
ambapo mkoa wa Kagera umewakilishwa na Mkuu wa Mkoa wa huo Meja Jenerali
Mstaafu Salim Kijuu.
Wananchi
wa mkoa wa Shinyanga wameguswa na kadhia iliyopata wananchi wa Kagera, hivyo
tukaamua kukusanya nguvu ya pamoja kama mkoa ili kuwafariji Watanzania wenzetu
kutokana na matatizo waliyoyapata” alisema Bi Zainabu.
Mkuu
huyo wa mkoa alifafanua mchango wa misaada waliyotoa kuwa ni paamoja na mabati
ya geji 28 1400, saruji mifuko 750, mchele kilo 600, mahindi kilo 100 paamoja
na nguo.
Bi.
Zainabu aliongeza kuwa michango ya msaada huo imeunganishwa nguvu kutoka
Serikali ya mkoa wa Shinyanga, taasisi za Serikali na zisizo za kiserikali,
sekta binafsi, masshirika ya dini, asasi za kiraia, wafanyabiashara, mogodi ya
madini iliyopo mkoani humo na wadau wengine wa maendeleo.
Akitoa
shukrani mara baada ya kupokea msaaada huo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali
Mstaafu Kijuu amewashukuru wananchi wa
Shinyanga kwa kuwafariji, majitoleo yao kwana kuwajali katika kipindi hiki cha
mpito cha athari za tetemeko lililoukumba
mkoa huo.
|
0 comments:
Post a Comment