Home » » Mwenyekiti kortini akituhumiwa kuua vikongwe

Mwenyekiti kortini akituhumiwa kuua vikongwe

 

By Shija Felician, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz
Kahama. Polisi wamemfikisha mahakamani Mwenyekiti wa Kijiji cha Chambo, Clement Shija kwa tuhuma za mauaji ya vikongwe wawili kwa imani za ushirikina.
Awali, mwenyekiti huyo alitoroka baada ya kutokea kwa mauaji hayo, hali iliyosababisha polisi kuendesha msako uliofanikisha kumkamata.
Akimsomea mashtaka mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kahama, Kenedy Mtembe, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Peter Masatu alidai kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Agosti baada ya mtoto wake kufariki dunia.
Masatu alidai mshtakiwa baada ya kufiwa na mtoto, aliongoza na mamia ya wanakijiji wenzake kwenda kuwashambulia vikongwe hao kisha kuwateketeza kwa moto.
CHANZO GAZETI LA MWANANCHI 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa