Benjamin Sawe
Maelezo
Wanadamu wameumbwa kwa hulka na silika ya kuwa na uwezo wa
kuwasiliana miongoni mwao, jamii wanamoishi, taifa na hata ulimwenguni ili
waweze kutimiza nia na azma yao ya kuwasiliana.
Ili mawasiliano hayo yakamilike ni lazima yabebe ujumbe
unaokusudiwa kufikishwa katika jamii.
Ujumbe huo ili uweze kumfikia mlengwa, ni lazima iwepo njia ya
kuufikisha ujumbe huo kwa mlengwa ambao huwasilishwa kwa maandishi (magazeti),
sauti (redio) na picha (TV) pamoja na mitandao ya kijamii kupitia huduma ya
inteneti.
Vyombo hivyo vya habari vinahusisha wataalamu ambao kazi yao ni
kuhakikisha jamii inapata ujumbe kwa wakati ili kuweza kujenga, kuboresha na
kuimarisha maisha yao kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni.
Vyombo vya habari hakika vimekuwa ndio macho na masikio ya
wananchi ili kufikisha ujumbe unaohusu mambo mbalimbali yanayofanyika ndani na
nje ya nchi.
Uanzishwaji
wa Bodi ya Ithibati ya Wanahabari kama ilivyoainishwa katika Muswada wa Huduma
za Habari wa mwaka 2016 hautaminya uhuru wa kutafuta na kusambaza habari.
Msingi wa
haki ya kutafuta taarifa na kusambaza habari unatokana ibara ya 18 ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo watu wasiwe na hofu ya kuwa Bodi hiyo
itawaminya watu kutoa mawazo yao.
Bodi ya
Ithibati ya Wanahabari haiwezi kuwa kizuizi cha watu kutafuta na kusambaza
habari kwani haki hiyo ipo kikatiba kupitia ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania
Sioni sababu
yoyote ya kupinga uanzishwaji wake kwa kuwa malengo yake ni kuhakikisha
inasimamia kanuni za maadili ya wanahabari hapa nchini na kuijengea heshima
tasnia.
Pamoja na
kuanzishwa kwa Bodi hiyo hakuna maana kwamba uanzishwaji wake utachukua
majukumu ya taasisi zingine za habari zilizopo na kuongeza kuwa waandishi wa
habari duniani kote wanafanya kazi kwa kufuata miiko ya maadili ya uandishi wa
habari.
Suala
kubwa kwa mwanahabari ni kuzingatia maadili na weledi wa taaluma yake ili
kutekeleza majukumu yake pasipo kusababisha usumbufu kwa mtu au kikundi kingine
Muswada huu umeandaliwa kukabiliana na
changamoto mbalimbali zilizopo katika tasnia ya habari nchini ambazo ni pamoja
na upungufu wa sheria zinazosimamia tasnia hii na mabadiliko ya teknolojia ya
habari.
Changamoto ya kutokuwepo kwa udhibiti
mzuri na usimamizi madhubuti ya viwango kwenye taaluma ya habari na utangazaji
kumechangia madhila kwa jamii ikiwemo kuandikwa habari za upotoshaji,
zinazokiuka maadili na zinazoweza kusababisha chuki, machafuko na uvunjifu wa
amani.
Kutokana na mwingiliano wa teknolojia,
mwaka 2003 serikali iliona umuhimu wa kuunganisha vyombo viwili; Tume ya
Mawasiliano na Tume ya Utangazaji ili kuleta ufanisi wa usimamizi wa sekta na
utoaji wa huduma bora kwa walaji.
Kwa ujumla sekta hii changamoto kubwa
ni taaluma ya habari kutotambulika kama taaluma kamili inayopaswa kuheshimiwa,
kukosekana vyombo madhubuti na huru vya usimamizi na badala yake mambo mengi
kuwa chini ya serikali moja kwa moja
Sheria hii inaleta mageuzi makubwa
katika usimamizi wa sekta ya habari hapa nchini ni sheria ambayo inakwenda kwa
mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu, kuifanya rasmi sekta ya habari
kuwa sekta rasmi.
Wengi wamekuwa waathirika wa uandishi
usiozingatia maadili na weledi wa taaluma ya habari na utangazaji kwa
kukashifiwa au kuzushiwa taarifa zisizokuwa na ukweli wowote.
Mapendekezo yaliyomo katika sheria ya
habari kwa kiasi kikubwa yamelenga kutatua changamoto ya kuwa na wanahabari
waliosomea kazi yao na ambao wamewekeana maadili ya kufuata.
Ni sheria itakayoleta mifumo ya kisasa
ya usimamizi na ni mifumo ambayo inaweza kugusa au kubadili namna
tutakavyotenda na tunavyofikiria sasa,
Niwaombe wanatasnia wenzangu tuwe
tayari kwa mabadiliko ili taaluma yetu iheshimiwe na sisi wenyewe tuheshimike
zaidi.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment