Hapa ni katika viwanja vya Ofisi ya Mtendaji Kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga ambapo leo Jumamosi Februari 11,2017 Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amekabidhi vifaa tiba kwa mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kuvisambaza katika zanahati na hospitali zilizopo katika manispaa hiyo.
Vifaa tiba hivyo vimetolewa na Watanzania waishi nchini Denmark ambapo upatikanaji wa vifaa hivyo unatokana ushirikiano wa Diwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi (CHADEMA) na shirika la AGAPE la Mjini Shinyanga kuwasiliana Watanzania waishio nchini Denmark kisha kuleta vifaa hivyo.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo,Mkurugenzi wa shirika la AGPAE John Myola alisema wazo la kutafuta vifaa tiba lilitolewa na diwani wa kata ya Ngokolo Diwani Emmanuel Ntobi ambaye anajuana na watanzania waishio nchini Denmark.
“Diwani huyu alitupatia mawasiliano ya watu hao wanaojulikana Denish Relief Group kisha sisi kama shiriki tukaandika andiko tukiomba kupewa vifaa tiba kwa ajili ya kupunguza uhaba wa vifaa tiba katika zahanati na hospitali za manispaa ya Shinyanga”,alisema Myola.
Myola alitumia fursa hiyo kuiomba ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga kuhakikisha kuwa vifaa tiba hivyo vinatumika kama inavyotakiwa na kuhakikisha vinatunzwa.
Naye Diwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi alisema watanzania waishio Denmark wametoa vifaa tiba hivyo bure kwa ajili ya watanzania huku akiishukuru serikali kuruhusu vifaa hivyo kuingia nchini bila kulipiwa kodi.
“Hili jambo la kidiplomasia kwa nchi hizi mbili Tanzaia na Denmark,Denish Relief Group ni kundi la watu la kwanza kutoa msaada mkubwa nchini,huu ni kama mwanzo tu,wamesema wataendelea kutoa msaada na wamesema wapo tayari kutujengea zahanati katika kata hii ya Ngokolo ambayo haina zahanati”,alisema Ntobi.
“Tumepokea vifaa tiba aina 26,vimo vitanda,magodoro,viti vya kisasa vya wagonjwa,mashine ya Utra sound,mashine ya Incubation na vifaa vingine vingi ambavyo vitatumika katika kutoa huduma za afya kwa wananchi wa manispaa ya Shinyanga”,aliongeza Ntobi.
Hata hivyo diwani huyo aliomba vifaa hivyo vitumike vizuri na vitumike kwa wananchi wenye kipato cha hali ya chini.
Alisema pamoja na kutoa vifaa tiba,pia watanzania hao waishio nchini Denmark wametoa baiskeli kwa watu wenye ulemavu na nguo kwa makundi ya watu wasiojiweza wakiwemo wazee wanaolelewa katika kituo cha Kolandoto kilichopo katika manispaa ya Shinyanga.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika makabidhiano hayo,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alipongeza jitihada zilizofanywa na shirika la AGAPE na diwani wa kata ya Ngokolo katika kupatikana kwa vifaa hivyo.
“Hili ni tukio kubwa na la busara sana,limetutia moyo ,nawapongeza sana watanzania waishio Denmark na wote mliofanikisha kupatikana kwa vifaa hivi ambavyo vitakuwa msaada mkubwa kwa wananchi,huu siyo muda wa kufanya siasa,kinachotakiwa ni kuwaletea maendeleo wananchi bila kujali itikadi za kichama”,alieleza Matiro.
“Katika suala la maendeleo,serikali ipo tayari kushirikiana na shirika,kundi lolote la watu na hata mtu binafsi,tusitumie majukwaa ya maendeleo kufanya siasa,nimpongeze diwani wa kata hii kwa ushirikiano aliotuonesha katika kuwasaidia wananchi”,aliongeza Matiro.
Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo wakati wa makabidhiano hayo ametuletea picha 30 za matukio..Tazama hapa chini
Vifaa tiba vilivyotolewa na watanzania waishio nchini Denmark kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma za afya katika zahanati na hospitali zilizopo katika manispaa ya Shinyanga
Vifaa vya kufanyia mazoezi na viti vya kubebea wagonjwa
Vifaa tiba mbalimbali ikiwemo magongo,viti vya kuogea
Vifaa tiba vikiwa katika viwanja vya ofisi ya Afisa mtendaji kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga
Baiskeli za wagonjwa na vifaa tiba vingine vya kisasa
Vitanda vya wagonjwa
Vitanda vikiwa na magodoro yake
Afisa Mtendaji wa kata ya Ngokolo William Ndila akitambulisha wageni mbalimbali waliohudhuria hafla fupi ya kukabidhi vifaa tiba vilivyotolewa na watanzania waishio nchini Denmark "Denish Relief Group" kutokana na jitihada zilizofanywa na diwani wa kata hiyo Emmanuel Ntobi na Shirika la AGAPE
Mkurugenzi wa shirika la AGAPE la Mjini Shinyanga John Myola akizungumza katika hafla hiyo
Wananchi wakiwa eneo la tukio
Aliyesimama ni Mkurugenzi wa shirika la AGAPE la Mjini Shinyanga John Myola akielezea namna vifaa tiba vilipatikana kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma za afya kwa wananchi wa manispaa ya Shinyanga
Diwani wa kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga Emmanuel Ntobi(Chadema) akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba hivyo.Kushoto ni diwani wa viti maalum Zainab Heri (Chadema).Kulia ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Diwani wa kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga Emmanuel Ntobi(Chadema) aliwashukuru viongozi wa serikali kwa kuruhusu vifaa tiba hivyo kuingia nchini bila kodi huku akiomba serikali kuwapatia eneo kwa ajili ya kujenga zahanati katika kata hiyo ambayo haina zahanati kutokana na kushindwa kujenga baada ya kuibuka mgogoro kwenye eneo ambapo kulitakiwa pajenge zahanati
Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Magendi Magenzi ambaye ni afisa utumishi wa manispaa hiyo,akizungumza katika hafla hiyo ambapo kwa namna ya pekee alimpongeza diwani wa kata ya Ngokolo kwa jitihada alizofanya katika upatikanaji wa vifaa tiba hivyo.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Ngokolo John Nangi akizungumza wakati wa hafla hiyo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa hafla hiyo ambapo alisema serikali inaunga mkono jitihada zinazofanywa na wadau mbalimbali katika kuwaletea maendeleo wananchi
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika hafla hiyo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza umuhimu wa kuendeleza siasa kwenye masuala ya maendeleo
Diwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi akimwonesha mkuu wa wilaya vifaa tiba hivyo ikiwemo vifaa vya kubebea watoto na vifaa vya kufanyia mazoezi
Diwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi akiendelea kumwonesha mkuu wa wilaya ya Shinyanga vifaa tiba,pichani ni meza za kulia chakula na kabati
Diwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi akionesha vifaa tiba
Diwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi akiwa ameshikilia fimbo za watu wasioona
Baada ya kukabidhi baiskeli kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa viungo,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akishikana mkono na Richard ambaye ni mlemavu wa viungo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisalimiana na kijana mwenye ulemavu wa viungo baada ya kumkabidhi baiskeli
Wananchi wenye ulemavu wa viungo wakiwa wamekaa kwenye baiskeli
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na mkurugenzi wa shirika la AGAPE John Myola wakiwasindikiza wananchi wenye ulemavu wa viungo baada ya kuwapatia baiskeli hizo.Baiskeli hizo zinaendelea kutolewa kwa wananchi mbalimbali wenye ulemavu wa viungo
Mashine ya Utra Sound ambayo pia imetolewa na watanzania waishio Denmark
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza baada ya kuona mashine mbili Utra Sound kwa ajili ya akina mama wajawazito na Mashine ya kukuzia watoto njiti
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza baada ya kuona mashine za kisasa za kutolea huduma za afya
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
0 comments:
Post a Comment