Daktari wa Kinywa na Meno Hospitali ya Huruma CDH ya Mkoani Kilimanjaro Sr, Benjamine Buya (kushoto) akimfanyia uchunguzi wa Afya ya Kinywa na Meno Mwanafunzi wa Darasa la 3 wa Shule ya Msingi Jumuishi ya Buhangija Mkoani Shinyanga, Tausi Yanssni , anayeshuhudia (katikati) ni Mwalimu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Profesa Bakari Lembariti
Daktari wa Kinywa na Meno Hospitali ya Huruma CDH ya Mkoani Kilimanjaro Sr, Benjamine Buya (kushoto) akimfanyia uchunguzi wa Afya ya Kinywa na Meno Mmoja wa wanafunzi wanaosoma katika Shule hiyo jana
Maktari Bingwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Habiba Madjapa (kushoto) akimfanyia uchunguzi wa Afya ya Kinywa na Meno mwanafunzi wa Shule hiyo, kulia ni Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno, Tanzania Dr. Lorna Carneiro
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Jumuishi ya Buhangija Mkoani Shinyanga wakipiga mswaki mara baada ya kufanyiwa uchunguzi wa Afya ya Kinywa na Meno
Wanafunzi Wenye ulemavu wa kutosikia wakizungumza jambo wakati Madaktari wa Afya na Kinywa na Meno walipokuwa wakifanya uchunguzi wa Afya ya Kinywa na Meno katika Shule ya Buhangija mkoani Shinyanga
Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania, Dr. Lorna Carneiro (wa pili kushoto) akizungumza jambo na mtoto moja ambaye anasoma katika Shule hiyo,
Na Khamis Mussa, Shinyanga.
ambapo aliweza kusema, napenda kuwashukuru wenyeji wetu kwa ushirikiano waliotupa na kuwashukuru madaktari wote waliojitokeza katika kusaidia kutowa huduma kwa watoto wote na kwa jamii nzima bila kuchoka nakuwaomba wahisani kujitokeza kusaidia kupambana na magonjwa ya Kinywa na Meno kwa watoto hao, Carneiro alisema, amepata faraja yakuona tofauti ya watoto hao ni kubwa sana tofauti na mwaka wakwanza walipofika Kituoni hapo.
Kadri wanavyo endelea kuja anaona afya za watoto hao zinazidi kuimarika kutokana na Elimu wanayoendelea kuitoa kwa watoto hao kwa utumiaji na upigaji mswaki, inaonyesha elimu wanayoendelea kuitowa inazingatiwa katika utunzaji wa afya ya kinywa na meno na elimu wanayoendelea kuitowa ina wasaidia katika utunzaji wa hali ya afya zao za kinywa na meno,
Carneiro aliendelea kusema, MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana anatarajiwa kuongoza
matembezi ya Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno yatakayofanyika mkoani humo Machi 19 mwaka huu.Matembezi hayo yatafanyika katika Viwanja vya Nyerere Square na uwashirikisha wadau mbalimbali wa sekta ya afya na wananchi wa mkoa huo kwa kupata huduma ya afya ya kinywa na meno bure . aliesma
wamepanga kuwa na matembezi ya uhamasishaji wa jamii kuhusu umuhimu
wa afya ya kinywa na Meno tarehe 19 Machi, eneo ya Nyerere Square, Dodoma.
Sanjari na matembezi hayo siku itakayofuata Machi 20, ambayo itakuwa ni kilele cha wiki ya Afya ya Kinywa na Meno Tanzania na Siku ya Afya ya Kinywa na Meno Duniani, kutakuwa na uchunguzi wa afya ya kinywa ya meno kwa wananchi bila malipo na katika maadhimisho hayo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi, George Simbachawene.
Mkuu wa Kituo ambaye ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Buhangija Seleman Kipanya, akieleza hali ilivyokuwa kabla ya jopo la Madaktari kufika na kutowa elimu ya Afya ya Kinywa na Meno kwakuwachunguza na kutibu watoto waliogundulika na matatizo mbalimbali, aliyasema hayo, Kipanya, wakati wa Wiki ya Kinywa na Meno kwa
Mwanzoni katika mwaka wa kwanza kulikuwa na matatizo mengi ambayo yaliyokuwa yanawakabili vijana ikiwa ni pamoja na kutoboka kwa meno ambapo hawakuwa na namnabora ya kusafisha meno , lakini kwa mwaka wa kwanza baada ya kutowa elimu ya kinywa na kuwafanyia uchunguzi na kutowa ushauri na mwaka uliofatia kulikuwa na mabadiliko makubwa na kwamwaka huu tulionao kiukweli kumekuwa na mabadiliko makubwa sana
0 comments:
Post a Comment