Wahasibu zaidi ya 130 kutoka halmashauri za wilaya za mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kati wamepatiwa mafunzo ya Mfumo wa Kielekroniki kuhusu Usimamizi wa fedha ngazi za msingi zikiwemo zahanati,vituo vya afya,hospitali na shule za msingi na sekondari.
Mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and Reporting System – FFARS) kupitia mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ‘ Public Sector Systems Strengthening – PS3’ unaotarajiwa kuanza kutumika Julai 1,2017 katika halmashauri mbalimbali nchini.
Wahasibu hao wanashiriki katika mafunzo yanayofanyika katika ukumbi wa Vigimark Hotel Mjini Shinyanga ambayo yamekutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishi kutoka PS3,TAMISEMI,Wizara ya afya,wizara ya elimu.
Mwezeshaji wa Mafunzo hayo, Elizeus Rwezaula ambaye ni Mshauri wa Masuala ya Usimamizi wa Fedha za Umma kutoka Mradi wa HPSS Dodoma,alisema mfumo wa kutumia njia za kielektroniki (kompyuta) katika kuingiza taarifa za kifedha za vituo vya kutolea huduma unasaidia kurahisisha kazi.
“Katika Afrika Mashariki,Tanzania ndiyo nchi pekee itakayoanza kutumia mfumo huu wa kisasa wa kielektroniki katika uingizaji taarifa za fedha katika ngazi za msingi za kutolea huduma,na umetengezwa na vijana wa hapa nchini ili kuhakikisha kuwa mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma (FFARS) unafanikiwa”,alieleza Rwezaula.
“Tunawashauri wale wanaoendelea kutumia mfumo wa zamani wa ujazaji taarifa kwa kutumia vitabu (manual) waanze kutumia mfumo huu mpya wa uingizaji taarifa kwa mfumo wa kompyuta ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia”,aliongeza Rwezaula.
Kwa upande Mkuu wa Idara ya Ufuatiliaji,Tathmini na Tafiti Tendaji kutoka PS3, Dk. Suma Kaare alisema mfumo wa ujazaji taarifa kwa njia ya kieletroniki ulipendekezwa na PS3 na tayari serikali imeukubali na utaanza kutekeleza mwezi Julai,2017 katika halmashauri mbalimbali.
Naye Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi TAMISEMI, Elisa Rwamiago alisema baada ya wahasibu hao kupatiwa mafunzo kuhufu FFARS nao wataenda kutoa elimu kuhusu mfumo kwa watoa huduma wengine wa ngazi za chini.
Mafunzo ya siku mbili kuhusu mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma (FFARS) kupitia mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) yamemalizika leo mjini Shinyanga.
TAZAMA PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA MAFUNZO
Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi TAMISEMI, Elisa Rwamiago akizungumza wakati wa mafunzo kuhusu mfumo huo kupitia mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ‘ Public Sector Systems Strengthening – PS3’ unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID)
Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi TAMISEMI, Elisa Rwamiago akielezea kuhusu mfumo wa kielektroniki katika ujazaji taarifa za fedha katika vituo vya kutolea huduma.
Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi TAMISEMI, Elisa Rwamiago akizungumza ukumbini
Mwezeshaji wa Mafunzo ya FFARS ,Elizeus Rwezaula ambaye ni Mshauri wa Masuala ya Usimamizi wa Fedha za Umma kutoka Mradi wa HPSS Dodoma,akitoa mada kuhusu njia/mfumo wa kielektroki katika ujazaji taarifa za fedha katika vituo vya kutolea huduma
Mwezeshaji wa mafunzo hayo,Elizeus Rwezaula akionesha kwa vitendo namna ya kujaza taarifa za fedha kwa kutumia njia ya kompyuta/kielektroniki
Muonekano wa sehemu ya kujazia taarifa katika kompyuta
Mwezeshaji wa mafunzo hayo,Elizeus Rwezaula akiendelea kutoa somo
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Bwana Elizeus Rwezaula akizungumza ukumbini
Mkuu wa Idara ya Ufuatiliaji,Tathmini na Tafiti Tendaji kutoka PS3, Dkt. Suma Kaare akizungumza ukumbini ambapo alisema mfumo wa ujazaji taarifa kwa njia ya kielektroniki ulibuniwa na PS3 kisha kuwasiliana na serikali ambayo kwa pamoja wameamua kutekeleza mfumo huo katika halmashauri mbalimbali nchini
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo akijifunza kwa vitendo jinsi ya kuingiza taarifa za fedha kwa njia ya kielektroniki
Washiriki wa mafunzo hayo wakijifunza kwa vitendo namna ya kujaza taarifa za fedha kwa kutumia kompyuta
Mwenyekiti wa mafunzo hayo ya FFARS ,Samson William akizungumza ukumbini wakati akiendesha majadiliano mbalimbali
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano PS3, Leah Mwainyekule akielezea utaratibu utakaotumika kwa wakufunzi waliopata mafunzo ya FFARS watakavyokwenda kutoka elimu kuhusu FFARS katika vituo vya kutolea huduma
Kabla ya kufundishwa njia ya kieletroniki katika kujaza taarifa za fedha,washiriki wa mafunzo hayo wakiwa katika kikundi wakijadili namna ya kujaza taarifa kwa njia ya zamani ya kutumia vitabu.Walijadili namna ya kutunza kumbukumbu za miamala ya kifedha na nyaraka kwa kutumia vitabu
Washiriki wakiendelea na kazi ya vikundi.Washiriki hao walijifunza pia namna ya kuandika miamala ya kifedha kwenye nyaraka na vitabu vya uhasibu.
Mkuu wa Idara ya Ufuatiliaji,Tathmini na Tafiti Tendaji kutoka PS3, Dkt. Suma Kaare akifunga mafunzo ya mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and Reporting System – FFARS) kupitia mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ‘ Public Sector Systems Strengthening – PS3’ yaliyofanyika kwa siku mbili kuanzia Juni 5,2017- Juni 6,2017katika ukumbi wa Vigirmark Hotel mjini Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
0 comments:
Post a Comment