Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mgeni Kaimu Mratibu wa Ukimwi mkoa wa
Shinyanga Sherida Madanka akizungumza wakati wa kufungua Malumbano ya
Hoja kwa vijana yaliyoandaliwa na shirika la AGPAHI leo Ijumaa Julai
28,2017.
Vijana wakiwa ukumbini
Dk. Kashumba akisisitiza jambo ukumbini.
Kushoto ni mwenyekiti wa Malumbano hayo
ya hoja akifuatiwa na Mtoa huduma za afya katika kituo cha afya
Kambarage halmashauri ya Shinyanga Glory Assey na Mtoa huduma za afya
kutoka wilayani Kishapu Mwanaisha Nguya wakifuatilia kilichokuwa
kinaendelea ukumbini.
Mwenyekiti/Kijana aliyekuwa anaongoza malumbano ya hoja kwa vijana.
Kijana akichangia hoja ukumbini.
.
Kijana akichangia hoja ukumbini.
Wafanyakazi wa shirika la AGPAHI wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini.
Kijana akizungumza wakati wa malumbano ya hoja.
Watoa huduma za afya wakiwa ukumbini.
Kijana akichangia hoja ukumbini.
Kila mshiriki wa Malumbano ya Hoja alipewa zawadi ya begi la shule: Katikati
ni Kaimu Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Shinyanga Sherida Madanka
akimkabidhi mabegi mmoja wa vijana walioshiriki malumbano ya hoja ili
awagawie wenzake.
Kaimu Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Shinyanga Sherida Madanka akiendelea kugawa mabegi kwa vijana hao.
Zoezi la kugawa mabegi kwa vijana likiendelea.
Kaimu Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Shinyanga Sherida Madanka akifunga Malumbano ya hoja kwa vijana.
Picha ya pamoja mgeni rasmi,wafanyakazi wa shirika la AGPAHI na vijana walioshiriki katika malumbano ya hoja.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Mratibu wa Masuala ya Watoto AGPAHI mkoa
wa Shinyanga,Dk. Jane Kashumba akizungumza wakati wa Malumbano ya Hoja
kwa vijana yaliyoandaliwa na shirika hilo katika ukumbi wa Karena Hotel
mjini Shinyanga.
*****
Ijumaa Julai 28,2017 Vijana wamekutana
katika Ukumbi wa Karena Hotel mjini Shinyanga kwa ajili ya Malumbano ya
Hoja kuhusu Vijana kujadili kuhusu utaratibu wa kupambana na kudhibiti
maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU),unyanyapaa na vifo
vinavyotokana na Ukimwi nchini Tanzania.
Malumbano hayo ya Hoja yaliyoandaliwa na
shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI)
linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi
kupitia kwa ufadhili wa mfuko wa kusaidia Watoto wenye VVU Kwa hisani ya
watu wa Uingereza (CIFF) yamekutanisha vijana kutoka wilaya ya
Kahama,Kishapu na Shinyanga.
Wakichangia hoja,vijana hao mbali na
kulipongeza shirika la AGPAHI na serikali katika kuboresha huduma za
afya katika vituo vya kutolea huduma pia waliishukuru AGPAHI kwa
kusaidia watu wanaoishi na maambukizi ya VVU.
Vijana hao walisema ili kuhakikisha
mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi yanafanikiwa ni vyema suala la elimu
kuhusu Ukimwi likatiliwa mkazo katika maeneo yote mjini na vijijini
kwani vifo vingi vinatokea kutokana na jamii kutokuwa na elimu sahihi.
“Elimu sahihi kuhusu Ukimwi bado
haijatolewa kwa pande zote mbili za watu wanaoishi na maambukizi ya VVU
na wale wasio na maambukizi ya VVU,elimu ikitolewa watu hawatapata
maambukizi mapya,watu watazingatia matumizi sahihi ya dawa na hapatakuwa
na unyanyapaa”,walieleza vijana hao.
“Watu hawajitokezi kupima afya zao hali
ambayo inachangia kuwepo kwa vifo vinavyotokana na Ukimwi,watu hao
wangepata elimu sahihi wangeweza kuanza kutumia dawa za kupunguza makali
ya VVU lakini kutokana na kutojua afya zao wengine wanakuwa na imani za
kishirikina kwamba wamerogwa kumbe wamejiroga wao wenyewe kwa kutopima
afya zao”,waliongeza vijana hao.
Katika hatua nyingine vijana hao
waliitaka serikali kuboresha mazingira katika shule kwa kuwajengea
mabweni wanafunzi wa kike ili kuwaepusha na vishawishi wanaposafiri
umbali mrefu kutoka majumbani kwao kwenda shuleni.
“Tunaomba wanafunzi wajengewe mabweni
kwani wapo wanafunzi wanaopata vishawishi wakiwa njiani lakini wengine
kutokana na hali ngumu ya maisha wanajikuta wanaingia katika mahusiano
ya kimapenzi matokeo yake wanapata maambukizi ya VVU”,walisema.
Naye Mratibu wa Masuala ya Watoto AGPAHI
mkoa wa Shinyanga,Dk. Jane Kashumba alisema lengo la Malumbano hayo ya
Hoja ni kutaka kujua vijana wanahitaji nini ili kuhakikisha mapambano
dhidi ya VVU na Ukimwi yanafanikiwa nchini Tanzania.
“Sisi tunajihusisha na mapambano dhidi
ya maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto,tunatamani kuona
watoto wote walio na maambukizi wanapata huduma za afya lakini pia
kuhakikisha vijana wanatumia dawa na wale vijana waliopo katika jamii
wanapima afya zao”,alieleza Dk. Kashumba.
“Tunatambua uwepo wa vijana ndiyo maana
tumeona ni vyema tuwe na Malumbano ya hoja na vijana ili tuweze kujua
wanaelewa kiasi gani kuhusu huduma rafiki zinazopatikana katika vituo
vyetu vya kutolea huduma na pia tuone je wanaonaje utaratibu wa
kupambana na kudhibiti maambukizi mapya ya VVU,unyanyapaa na vifo dhidi
ya Ukimwi kama unafanyika ipasavyo nchini”,aliongeza Dk. Kashumba.
Akizungumza wakati wa Malumbano hayo ya
Hoja,Mgeni Kaimu Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Shinyanga Sherida Madanka
alisema malumbano hayo ni fursa nzuri kwa vijana kujieleza na kutoa
maoni yao nini kifanyike katika mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi katika
jamii.
“Nawapongeza sana vijana kwa uwezo
mlionao wa kujieleza katika masuala ya VVU na Ukimwi naamini kupitia
elimu hii ya kutosha mliyonayo mtaitumia kuielimisha jamii ili
kuhakikisha kuwa maambukizi mapya yanapungua”,alieleza Madanka.
Katika hatua nyingine Madanka aliwasihi
watu wanaoishi na VVU kujiamini sambamba na kuwa wafuasi wazuri wa dawa
ili kufikia malengo yao huku akiwasisitiza wananchi kujitokeza kupima
afya zao.
Shirika la AGPAHI linatekeleza shughuli
zake katika mikoa ya Shinyanga,Simiyu,Mwanza,Tanga,Geita na Mara kwa
ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia shirika la Centres for Disease
Control and Preventation (CDC),mfuko wa kusaidia Watoto wenye VVU Kwa
hisani ya watu wa Uingereza (CIFF) na Shirika la Development Aid From
People to People (ADPP - Mozambique).
0 comments:
Post a Comment