Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WANANDOA wamebainika kuwa vinara wa kupata maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi (VVU), kutokana na kutozingatia sheria na kanuni za ndoa.
Imedaiwa kwa sasa wamekuwa wakiingia kwenye ndoa kama fasheni na kujikuta mara baada ya miezi michache wakichokana na kufarakana, huku kila mmoja akianza kuwa na michepuko na hatimaye kusababisha familia yao kupata maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi.
Mwandishi wa kitabu cha ‘Sakramenti ya ndoa katika nyumba aminifu’, Paschal Maziku, alisema hayo wakati akikitambulisha kitabu hicho kwa waumini wa kanisa Katoliki Ngokolo, mjini Shinyanga, kabla ya kuzinduliwa rasmi na Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Liberatus Sangu.
Maziku ambaye ni mratibu wa programu ya nyumba aminifu kutoka Shirika la (maternal life intenational), tawi la Tanzania jijini Dar es Salaam, ambao wanajishugulisha na kutoa semina za masuala ya ndoa, zinazojenga misingi imara kwa watu
waliofunga pingu hizo za maisha, na wale ambao wanatarajia kufanya hivyo.
“Tulifanya utafiti na kugundua wanandoa ndio vinara wa maabukizi mapya ya virusi vya Ukimwi (VVU), kisheria wanandoa ndio wanapaswa kuwa salama sababu kabla ya kufunga pingu za maisha huwa wanapimwa afya zao, lakini kwa hali ya sasa imebadilika na wengi ndio waathirika wa Ukimwi,” alisema.
Alisema wakati wa kutoa semina hizo, watu waliomba waandikiwe kitabu kupata maarifa zaidi juu ya masuala ya ndoa.
Askofu Sangu, aliwaasa waumini hao kuendelea kutumia karama zao kuisaidia jamii, na kuwataka wanadamu wamkabidhi maisha yao Mwenyezi Mungu.

0 comments:
Post a Comment