Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Injinia Silvester Mahole akizungumza katika warsha ya kundi la wafanyabiashara wa hoteli na nyumba za kulala wageni mjini Shinyanga leo Ijumaa Agosti 4,2017. Kushoto ni mwenyekiti wa warsha hiyo Willium Shayo ambaye ni Mkurugenzi wa Evergreen Hotel ,kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya SHUWASA,Deogratius Sulla.
Mwenyekiti wa bodi ya SHUWASA,Deogratius Sulla akifungua warsha ya kundi la wafanyabiashara wa Hoteli na Nyumba za Kulala Wageni (Guest House and Logde) iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA) leo Ijumaa Agosti 4,2017.-Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Injinia Silvester Mahole akizungumza katika warsha ya kundi la wafanyabiashara wa hoteli na nyumba za kulala wageni mjini Shinyanga.
Injinia Mahole akizungumza katika warsha hiyo.Kushoto ni mwenyekiti wa warsha hiyo William ShayoWillium Shayo ambaye ni Mkurugenzi wa Evergreen Hotel,kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya SHUWASA,Deogratius Sulla.
Mwenyekiti wa warsha hiyo William ShayoWillium Shayo ambaye ni Mkurugenzi wa Evergreen Hotel akizungumza wakati wa warsha hiyo.
Shayo akizungumza ukumbini.
Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Injinia Silvester Mahole akielezea kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mamlaka hiyo.
Washiriki wa warsha hiyo wakisikiliza kwa umakini mada iliyokuwa inaendelea.
Warsha inaendelea.
Afisa Uhusiano wa SHUWASA,Nsianeli Gelard akielezea kuhusu Haki na Wajibu wa mteja wa SHUWASA ambapo aliwasisitiza wananchi kuwafichua watu wanaohujumu miundo mbinu ya mamlaka hiyo na kuwaasa kulipa ankara kwa wakati na kuepuka kutumia mafundi wa mitaani.
Sehemu ya mada ya Afisa Uhusiano wa SHUWASA,Nsianeli Gelard
Meneja Biashara wa SHUWASA, Reuben Mwandumbya akielezea kuhusu sheria inayohusu wizi wa maji.
Meneja wa Karena Hotel Richard Luhende akichangia hoja ukumbini.
Meneja Ufundi wa SHUWASA, Geofrey Hilly akizungumza ukumbini.
Meneja wa Kisindi Lodge Agnes Nyamwihula akichangia hoja katika warsha hiyo.
Meneja wa Katemi Hotel,Lameck Ntule akichangia hoja ukumbini.
Warsha inaendelea.
Afisa Rasilimaliwatu na Utawala wa SHUWASA,Kambira Mtebe ambaye alikuwa MC katika warsha hiyo akikisisitiza jambo ukumbini.
Wafanyakazi wa SHUWASA wakiwa ukumbini.
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Ijumaa
Agosti 04,2017 Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini
Shinyanga (SHUWASA) imekutana na kundi la wafanyabiashara wa Hoteli na
Nyumba za Kulala Wageni (Guest House and Logde) mjini Shinyanga kwa
lengo la kuwapa uelewa jinsi Mamlaka inavyojiendesha sambamba na kupata
maoni kutoka kwa wadau hao na kuweka mikakati ya pamoja ya kuboresha
huduma.
Akizungumza
katika kikao hicho,Mwenyekiti wa bodi ya SHUWASA,Deogratius Sulla
alisema utoaji wa huduma kwa wananchi una changamoto nyingi ambazo njia
pekee ya kuzitatua ni kushirikisha wadau wote.
“Mamlaka
imekuwa ikitoa elimu kwa wadau kuhusu namna mamlaka inavyojiendesha na
kadri wadau wanavyoelewa kuhusu haki na wajibu wao ndivyo wanavyoweza
kushiriki kikamilifu kutatua changamoto zinazojitokeza hivyo kuleta
mshikamano zaidi baina ya mamlaka na wadau wake”,alisema Mwenyekiti.
Wakichangia
hoja katika warsha hiyo,wafanyabiashara hao walisema kero kubwa
waliyohitaji ifanyiwe kazi haraka iwezekanavyo ni kukosekana kwa Mfumo
wa Majitaka hali inayosababisha watumie gharama kubwa kwa ajili ya
huduma ya kuondoa majitaka katika maeneo yao ya biashara.
Meneja
wa Karena Hotel Richard Luhende alisema kukosekana kwa mfumo wa
majitaka kunawasababishia hasara akitolea mfano wa hoteli hiyo kuita
magari ya majitaka walau mara tatu kwa wiki.
Naye
Meneja wa Kisindi Lodge Agnes Nyamwihula aliomba wafanyakazi wa mamlaka
hiyo kufanya kazi kwa uadilifu ikiwa ni pamoja na kusoma mita
zilizowekwa nje ya nyumba kwani baadhi ya mita huwa hazisomwi matokeo
yake Ankara ya maji inakuwa kubwa.
Kwa
Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Injinia Silvester Mahole
alisema mamlaka hiyo ipo katika mkakati wa kuwa na mfumo wa majitaka
mjini Shinyanga ingawa gharama za kuendeshea mradi wa majitaka ni kubwa.
“Tayari
tumeshapata eneo la kufanyia mradi huu,tunafanya jitihada za kutafuta
wafadhili,tatizo ni kwamba wafadhili wengi wanaogopa kuwekeza katika
mradi wa maji taka kutoka na gharama zake kuwa kubwa zaidi ya mradi wa
maji safi”,aliongeza Injinia Mahole.
Katika
hatua nyingine alitumia fursa hiyo kuwahamisha wateja wa mamlaka hiyo
kutumia njia za kisasa kulipia Ankara zao kama vile kulipa kwa njia ya
M-PESA,TIGO PESA au benki ya NMB au Benki ya CRDB.
“Tunawashauri
wateja wetu kubadilika kulingana na maendeleo ya sayansi na
teknolojia,tumeboresha huduma zetu kwa kiwango cha juu sana,mbali na
kulipa bill kwa njia ya simu,hivi sasa unaweza kulipa kwa njia ya
benki”,alieleza Injinia Mahole.
Injinia
Mahole alizitaja baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni
pamoja na gharama kubwa za uendeshaji,uhaba wa nyenzo za kufanyia
kazi,bomba za spea na presha kubwa ya maji kutoka Mradi wa Maji ya Ziwa
Victoria hali inayosababisha kupasuka kwa mabomba.
0 comments:
Post a Comment