Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
  
Dkt.Maeja akizungumzia masuala mbalimbali kuhusu Stand United.
Wananchi wakiwa katika mkutano huo.  Mheshimiwa Stephen Masele akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Dk. Maeja.
 Mheshimiwa Stephen Masele akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Dk. Maeja.
Diwani wa kata ya Kambarage katika manispaa ya Shinyanga,Hassan Mwendapolea akizungumza katika mkutano huo.
Wananchi wakiwa katika mkutano huo. Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Wakati
 pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2017-2018 likitarajiwa 
kufunguliwa rasmi kesho Agosti 27, mwaka huu kwa timu zote 16 kuingia 
viwanjani,Kampuni ya Michezo ya Bahati Nasibu Mtandaoni – BIKO 
imeidhamini Klabu ya Stand United ‘Chama la Wana’ shilingi milioni 100 
kuanzia mwaka huu.
Akizungumza
 katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo Ijumaa,Agosti 25,2017mjini 
Shinyanga, Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mheshimiwa Stephen Masele 
(CCM) alisema BIKO wameamua kuidhamini timu hiyo baada ya kuridhishwa na
 mwenendo wa timu hiyo. 
“Baada
 ya Stand United kupoteza mwelekeo na wadhamini wake Kampuni ya Acacia 
kujiondoa katika udhamini,hivi sasa nimeamua kuwa msimamizi mkuu wa timu
 hii,nimetafuta udhamini mwingine,nimeiomba kampuni ya Kitanzania ya 
BIKO,imekubali kuwa wadhamini wakuu na imetupatia shilingi milioni 100 
kwa mwaka huu”,alieleza Masele. 
Mbunge
 huyo alisema ameamua kuwa msimamizi mkuu wa timu hiyo ili kuhakikisha 
kuwa timu hiyo inafanya vyema katika michezo mbalimbali. 
“Najua
 mnaelewa uhusika wangu katika Stand United,mnafahamu jitihada 
nilizofanya kuhakikisha timu hii inafanya vizuri,ili timu hii iwe ya 
kimataifa na timu hii baada ya kupata matatizo yaliyotokea,ilikuwa kama 
timu yatima,haina ulezi,haina msaada,na mimi kama mbunge nilikuwa 
nimekasirika na nikasema Maeja na wenzake wasinisumbue katika mambo ya 
mpira”,alisema. 
“Nilitafuta
 ufadhili wa shilingi bilioni 2.4 kutoka Acacia,lakini tuliuchezea,na 
baada ya kujiridhisha na uongozi mpya ulioingia ukiongozwa na Dk. Maeja 
nimetafuta wadhamini wengine ambao ni kampuni ya BIKO ili kuisadia timu 
yetu,naomba fedha hizi zitumike vizuri”,alisema Masele. Masele alitumia 
fursa hiyo kuwatahadharisha viongozi wa timu kuhusu matumizi mabaya na 
ubadhirifu wa fedha zilizotolewa na wadhamini hao na kuwa hawatasita 
kuwachukulia hatua kali za kisheria.
“BIKO 
itapenda kuona fedha hizi zinatumikaje na kuanzia sasa mtu yeyote 
atakayejihusisha na ubadhirifu tutamfikisha katika vyombo vya sheria kwa
 sababu wanaumiza hisia za watu wengi”,aliongeza Masele. 
“Nataka
 niwahikikishie kuwa timu hii haitashuka daraja kinatochotakiwa ni kutoa
 msaada kwa timu hii ikiwemo kuishangilia,jambo jingine naomba mjitahidi
 kubana matumizi katika masuala mbalimbali ikiwemo pale mnaposafiri 
punguzeni idadi ya watu wa kusafiri lakini pia lipeni mishahara ambayo 
haiumizi sana”,aliongeza.
Kwa
 upande wake,Mwenyekiti wa Klabu ya Stand United,Dkt. Ellyson Maeja 
alisema Klabu hiyo ya Stand United imejipanga vizuri kuhakikisha kuwa 
inafanya vizuri katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2017-2018. 
"Hivi sasa timu imetulia kiuongozi tatizo ni bajeti,mpira ni pesa,bila 
pesa hakuna timu,lakini pia hatuna usafiri wala hosteli kwa ajili ya 
wachezaji,tunaomba wadau waendelee kujitokeza kuisaidia timu 
hii,tumesajili wachezaji wapya 19,jumla sasa wapo 30,tunaye kocha 
mzuri,walimu wazuri,malengo yetu ni kushika nafasi ya kwanza hadi ya 
tatu katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu wa 
2017-2018",alisema Dkt.Maeja. 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment