Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro leo amefungua mafunzo ya
“Tathmini ya Uwezo” kanda ya Shinyanga katika ukumbi wa Karena Hotel leo
Alhamis Oktoba 5,2017-Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo yatakayodumu kwa muda wa siku tatu.
Afisa Mawasiliano kutoka Jitihada ya Uwezo Twaweza,Greyson Mgoi akielezea kuhusu Tathmini ya Uwezo
Afisa Mawasiliano kutoka Jitihada ya Uwezo Twaweza,Greyson Mgoi akizungumza ukumbini.
Afisa Mawasiliano kutoka Jitihada ya Uwezo Twaweza,Greyson Mgoi akisisitiza jambo.
Mkurugenzi wa Shirika la OPE ambalo ni mdau wa Uwezo,William Shayo akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini.
Mkurugenzi
wa Shirika la OPE,William Shayo akielezea namna shirika lake
linavyoshirikiana na Twaweza kupitia zoezi la Tathmini ya Uwezo katika
kuboresha elimu kwa watoto.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini.
Mafunzo yanaendelea
Mafunzo yanaendelea.
Wadau wakiwa ukumbini.
Mwezeshaji katika mafunzo hayo Anandumi Ndosi akitoa mada wakati wa mafunzo hayo.
Mshiriki akinyoosha mkono ili aulize swali.
Washiriki wakifurahia jambo ukumbini.
Mwezeshaji katika mafunzo hayo Anandumi Ndosi akizungumza ukumbini.
Mafunzo yanaendelea.
Picha ya pamoja,washiriki wa mafunzo hayo na mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro.
Picha ya pamoja.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amefungua mafunzo ya “Tathmini
ya Uwezo” kanda ya Shinyanga ikiwa ni jitihada inayofanywa na shirika la
Twaweza kwa lengo la kupima uwezo wa watoto juu ya umahiri wao wa
kusoma,kuhesabu na kuandika.
Mafunzo
hayo yanayofanyika kwa muda wa siku tatu katika ukumbi wa Karena Hotel
Mjini Shinyanga,yameanza leo Alhamis Oktoba 5,2017.
Akizungumza
wakati wa mafunzo hayo,Afisa Mawasiliano kutoka Jitihada ya Uwezo
Twaweza,Greyson Mgoi akisema washiriki wa mafunzo hayo ni waratibu wa
wilaya na waratibu wa vijiji kutoka wilaya nane za kanda ya Shinyanga
inayojumuisha mikoa ya Dodoma,Singida,Simiyu na Shinyanga.
“Mafunzo
ya tathmini ya Uwezo yanafanyika nchi nzima na kwa upande wa kanda ya
Shinyanga,yanafanyika hapa ambapo tunafundisha mbinu na taratibu za
kufanya wakati wa kutekeleza zoezi la Tathmini ya Uwezo kwenye wilaya
mbalimbali nchini Tanzania na mwaka huu zoezi litafanyika katika wilaya
56”,alieleza Mgoi.
Alisema
washiriki wa mafunzo hayo watafundishwa namna ya kufanya tathmini
kuhusu uwezo wa watoto wenye kuanzia miaka 6 hadi 16 katika masomo
matatu ya Kiingereza,Kiswahili na Hesabu.
Aliongeza kuwa Twaweza kupitia tathmini ya uwezo imekuwa ikishirikiana na serikali katika kuboresha elimu nchini.
Naye
Mkurugenzi wa Shirika la OPE ambalo ni mdau wa Uwezo,William Shayo
alisema lengo la msingi la Uwezo ni matokeo ya kujifunza kwa watoto na
swali linaloulizwa kila siku ni “Je watoto wetu wanajifunza”.
“Tunatathmini
uwezo ujuzi wa watoto katika kusoma na kuhesabu,lakini pia kusambaza
matokeo ya utafiti sehemu kubwa kwa wananchi,wazazi,walimu na serikali
hali hii inasababisha wananchi wachukue hatua za kuboresha ngazi za
ujifunzaji za watoto kwenye jamii”,aliongeza.
Akifungua
mafunzo hayo,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alisema
serikali inatambua kazi nzuri zinazofanywa na taasisi katika kuboresha
sekta ya elimu na kwamba serikali itaendelea kushirikiana nao.
Aidha
Matiro aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kutoa taarifa kwa serikali
kuhusu mambo watakayoyabaini wakati wa tathmini yao ili kuisaidia
serikali kuboresha elimu katika maeneo yenye changamoto.
“Mkimaliza
kufanya tathmini mtuletee uhalisia,msituonee aibu kutuambia,tunahitaji
kujua uhalisia wa mambo kwamba watoto kweli wanaelewa?wanajua kusoma?
Hesabu wanazijua?,Mkileta tafiti zenu kwa uhalisia itakuwa rahisi kwa
wadau mbalimbali ikiwemo serikali kupata ufumbuzi wa matatizo katika
elimu kwa ajili ya kusaidia watoto”,aliongeza Matiro.
0 comments:
Post a Comment