Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu (Katikati), Afisa Kilimo na Mifugo Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Ayoub Sengo (Kulia), Mwingine ni Afisa Tawala Wilaya ya Ikungi Ndg Dandala Mzunguor.
Wataalamu wa kilimo, Mifugo, Ardhi, Maliasili na mazingira wakishauri jambo wakati wa kikao kazi na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu.
Wataalamu wa kilimo, Mifugo, Ardhi, Maliasili na mazingira wakishauri jambo wakati wa kikao kazi na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu.
Na Mathias Canal, Singida
Mkuu
wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amekutana na kufanya
kikao Cha kazi na wataalamu wa Kilimo, Mifugo, Ardhi, Maliasili na
mazingira kubaini kwa pamoja mbinu bora za kuwasaidia wakulima kuzalisha
mazao ya chakula na biashara kwa wingi.
Katika
kikao hicho kilichohudhuriwa na Maafisa kilimo na Mifugo, Maafisa
Ardhi, Maliasili na Mazingira, Maafisa Ugavi wa Kata sambamba na Maafisa
Tarafa, Mhe Mtaturu alisema kuwa bado uzalishaji wa mazao ni mdogo
katika Wilaya ya Ikungi ukilinganisha na hali ya hewa ikiwa ni pamoja na
kuwa na ardhi nzuri.
Aliwataka
wataalamu hao wa kilimo kuwasaidia wakulima ili kuiwezesha Sekta ya
Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kuwa kilimo cha kibiashara
kitakachowezesha kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na kupunguza umasikini
kwa watanzania Sambamba na kujitosheleza kwa chakula.
Mhe
Mtaturu alisema Ili kuwe na kilimo kizuri na tija kwa wananchi,
Wataalamu mnapaswa kuzingatia uwepo wa Pembejeo za kilimo na mbegu Bora
za kisasa ambazo zinazalisha mazao mengi sambamba na kuhuisha kilimo cha
umwagiliaji kwa kuandaa mpango wa kujenga skimu za umwagiliaji ili
wananchi waweze kuzalisha chakula cha kutosha mwaka mzima.
Alisema
kuwa ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo tayari serikali imetoa
tani 20 za mbegu za Pamba katika Wilaya ya Ikungi ambazo zitagawanywa
kwa wakulima ili msimu wa kilimo unapoanza tayari ukata wa kucheleweshwa
kwa mbegu hizo uwe umetekelezwa.
0 comments:
Post a Comment