Uongozi wa Shule
ya Msingi Kahama(B), iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama, umesema baada ya
siku tatu, utachukua hatua za kinidhamu
kwa wanafunzi watoro ambao wameshindwa kuhudhuria masomo, licha ya muhula wa kwanza wa masomo kuanza leo.
Akizungumza na Kijukuu
Blog, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, CONRAD
NKUBA amesema licha ya shule kufunguliwa, bado kuna baadhi ya wanafunzi
wameshindwa kuhudhuria masomo.
NKUBA amewataka
wazazi na walezi kuwahimiza wanafunzi kuhudhuria masomo na si kukaa nao na
kuwatumikisha shughuli za nyumbani.
Naye Mwalimu wa
Taaluma katika shule ya Msingi Majengo,
LETICIA BUCHUMA amesema katika
shule hiyo mahudhurio ya wanafunzi kwa
siku ya kwanza, ni mazuri ingawa bado kuna baadhi ya wanafunzi ni watoro.
Muhula wa Kwanza wa Masomo
katika shule za Msingi na Sekondari nchini, umeanza baada ya shule kufunguliwa rasmi leo Januari 8.
Kijukuu
0 comments:
Post a Comment