Home » » Halmashauri ya Kahama ya imeelezwa kuacha kuchukua tozo zisizo na umuhimu katika kipindi michezo yakunufaisha jamii.

Halmashauri ya Kahama ya imeelezwa kuacha kuchukua tozo zisizo na umuhimu katika kipindi michezo yakunufaisha jamii.



Anitha Jonas – MAELEZO,Kahama.
 

Kahama.
Halmashauri  ya Kahama ya imeelezwa  kuacha kuchukua tozo zisizo na umuhimu katika kipindi michezo yakunufaisha jamii.
Kauli hiyo imetolewa leo Mjini Kahama na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura alipokuwa akifunga mashindano ya Mbio za Baiskeli ya Tushikamane yaliyohusisha  Mikoa ya Kanda ya Ziwa na yamekuwa yakidhaminiwa na Kampuni ya Madini ya Acacia Buzwagi.
“Ombi langu kwenu Kampuni ya Acacia Buzwagi muongeze mkataba wenu wa kuwezesha mashindano haya kwa kuwa kupitia msaada wenu vijana hawa wa Kanda ya Ziwa wanapata kipato ambacho kinawasaidia katika maisha yao ya kiuchumi”,alisema Naibu Waziri Wambura.
Pamoja na hayo Naibu Waziri huyo alitoa rai kwa taasisi nyingine kujitokeza kusaidia  mashindano hayo ya ili kuweza kuwafikisha mbali wanamichezo hao wenye uwezo mkubwa wa kufanya mchezo huo kufikia hata kiwango cha Kimataifa.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Baiskeli Bw.Godfrey Mhagama alisema kwa mwaka huu kuna zaidi ya wachezaji 200 waliyoshiriki mshindano haya ombi langu kwa  serikali ifatafute wadau watakao weza kusaidia kuendeleza vipaji  vya vijana  hawa kanda ya ziwa iliwaweze kuufanya mchezo huu kuwa ajira na kupata mafanikiwa makubwa kama wachezaji wa ulaya.
“Wakazi wa Kanda ya Ziwa wa  wanauwezo mkubwa katika uendeshaji wa baiskeli  hii ni kutokana na utamaduni wao wa kutumia Baiskeli kama chombo cha usafiri”,alisema Bw.Mhagama.
Naye Meneja wa Mgodi wa Acacia  Buzwagi Bw.Asa Mwaipopo alisema katika mashindano hayo ya mwaka huu watatoa zawadi kuanzia mtu wa kwanza mpaka wa 30 na katika mashindano hayo wanaume watakimbia kilomita 156 na wanawake kilomita 80 na zawadi  ya mshindi kwanza kwa  mwanaume  ni milioni moja na nusu na kwa wanawake ni milioni moja.
Pamoja na hayo wanamichezo hao wameaswa kufanya juhudi katika mchezo huu pia kutojaribu kutumia madawa ya kuongeza nguvu wakati wa michezo.
              
                              *******************MWISHO********************


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa