Katibu
Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi.
Sihaba Nkinga akisalimiana na wazee alipotembelea Makazi ya kulea wazee
ya Kolandoto leo Mkoani Shinyanga.
Afisa
Mfawidhi wa Makazi ya Kulea Wazee ya Kolandoto Bi.Sophia Kang’ombe
akimkabidhi taarifa ya kituo hicho Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga wazee alipotembelea
Mkazi hayo leo Mkoani Shinyanga.
Afisa
Mfawidhi wa Makazi ya Kulea Wazee ya Kolandoto Bi.Sophia Kang’ombe
akimuleza Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Bi. Sihaba Nkinga (kulia) changamoto za Makazi hayo na
kumuomba kusaidia kusimamia utatuliwaji wa matatizo hayo ikiwemo ujenzi
wa majengo kwa ajili ya malazi ya wazee hao, Katikati ni Afisa Maendeleo
ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Bi. Amina.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi.
Sihaba Nkinga akiongea na Wazee wanaoishi katika Makazi ya Kulea Wazee
ya Kolandoto leo Mkoani Shinyanga na kuwahakikishia serikali kuendelea
kuwasaidia kutatua changamoto zinazowakabili ili kuwawezesha kuishi
katika mazingira rafiki. Katikati ni Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka
Wizara hiyo Bi. Amina… na kushoto ni Afisa Mfawidhi wa Makazi ya Kulea
Wazee ya Kolandoto Bi.Sophia Kang’ombe
Afisa
Mfawidhi wa Makazi ya Kulea Wazee ya Kolandoto Bi.Sophia Kang’ombe
akimuonesha Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga sehemu ya nyumba zinazohitaji ujenzi
kwa ajili ya Makazi ya Wazee hao. Wakati wa Ziara ya Kutembelea Makazi
ya Wazee na kuona hali halisi ya makazi hao.
Sehemu
ya Nyumba kwa ajili ya Makazi ya Wazee ambazo hazitumiki kutokana na
kuwa katika hali mbaya katika Makazi ya kulea Wazee ya Kolandoto Mkoani
Shinyanga.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi.
Sihaba Nkinga akizungumza na Mzee Samora Maganga ambaye ni Mwenyekiti wa
Wazee katika Makazi ya kulea Wazee ya Kolandoto Mkoani Shinyanga.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi.
Sihaba Nkinga akisalimiana na Wazee katika Makazi ya Kulea Wazee ya
Amani leo Mkoani Tabora.
Mganga
Mkuu wa Manispaa ya Tabora Dkt. Rashidi Said Akisoma taarifa ya kituo
cha Makazi ya kulea wazee ya Amani yaliyopo Mkoani Tabora kwa Katibu
Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi.
Sihaba Nkinga alipotembelea kituo hicho leo Mkoani Tabora ambapo mbali
na changamoto zinazokabili kituo hicho pia wamefanikiwa kutoa kadi za
Matibabu ya Afya za CHF kwa wazee wote kituoni hapo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi.
Sihaba Nkingaakimpa Zawadi ya Sabuni Mwenyekiti wa Kijiji cha Kolandoto
Bw. George Busambilo kwa niaba ya Wazee katika Makazi hayo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi.
Sihaba Nkinga akikagua Nyumba Wazoishi Wazee katika Mkazi ya Wazee ya
Amani leo Mkoani Tabora.
Na Hassan Silayo-MAELEZO
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi.
Sihaba Nkinga imeziasa Taasisi binafsi, Makampuni, Asasi za Kiraia na
watu binafsi kushirikiana na katika kutatua changamoto zinazokabili
makazi ya wazee na watu wenye ulemavu nchini.
Akiongea
wakati alipotembelea Makazi ya kulea wazee na watu wenye ulemavu ya
Kolandoto leo Mkoani Shinyanga Bi. Sihaba amesema kuwa ametembelea
baadhi ya makazi hayo na kuona yanahitaji msaada mkubwa hasa ujenzi wa
nyumba za malazi, umeme na madawa hivyo Taasisi binafsi, Makampuni,
Asasi za Kiraia na watu binafsi hawana budi kushirikiana na serikali
kamaliza kabisa changamoto hizo.
“nimetembelea
makazi kadhaa sasa, changamoto ni nyingi, wazee hawa wanahitaji msaada
mkubwa sana hivyo kwa nafasi hii natoa wito kwa Taasisi binafsi,
Makampuni, Asasi za Kiraia na watu binafsi kushirikiana na serikali
katika kuziondoa changamoto hizi katika makazi haya ili kuweza kuwafanya
wazee hawa kufurahia maisha katika makazi haya”.Amesema Bi. Sihaba.
Naye
Afisa Mfawidhi wa Makazi ya Kulea Wazee ya Kolandoto Bi.Sophia Kang’ombe
amewaomba wahisani na serikali kwa ujumla kusaidia katika ukarabati na
ujenzi wa majengo katika makazi hayo ili kupunguza changamoto ikiwemo
uvamizi wa vijana wanaotumia vilevi na bangi kuingia katika nyumba hizo
na kutishia kuwafanyia vitendo vibaya wazee wenye jinsia ya kike.
Akizungumza
kwa niaba ya Wazee katika Makazi ya Kolandoto Mkoani Shinyanga Mzee
Samora Maganga amesema kuwa kituo hicho kwa kiasi fulani kipo katika
hali nzuri ila wanaiomba serikali iwasaidie katika kutatua changamoto ya
umeme na majengo kwani imekuwa kero ya muda mrefu sasa.
Aidha
Bi. Sihaba akiongea na Wazee katika Makazi ya Amani Mkoani Tabora
aliwapongeza walezi wa makazi hayo kwa kuamua kutoa kadi za matibabu za
CHF kwa wazee hao na kushauri Walezi wa Makazi mengine ya Wazee nchini
kuiga mfano huo ili kusaidia katika utoaji bora wa huduma za afya kwa
wazee.
0 comments:
Post a Comment