Anitha Jonas –
MAELEZO,Kahama.
Kahama.
Halmashauri ya Kahama ya imeelezwa kuacha kuchukua tozo zisizo na umuhimu katika
kipindi michezo yakunufaisha jamii.
Kauli hiyo imetolewa
leo Mjini Kahama na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.
Anastazia Wambura alipokuwa akifunga mashindano ya Mbio za Baiskeli ya
Tushikamane yaliyohusisha Mikoa ya Kanda
ya Ziwa na yamekuwa yakidhaminiwa na Kampuni ya Madini ya Acacia Buzwagi.
“Ombi langu kwenu Kampuni
ya Acacia Buzwagi muongeze mkataba wenu wa kuwezesha mashindano haya kwa kuwa
kupitia msaada wenu vijana hawa wa Kanda ya Ziwa wanapata kipato ambacho
kinawasaidia katika maisha yao ya kiuchumi”,alisema Naibu Waziri Wambura.
Pamoja na hayo Naibu
Waziri huyo alitoa rai kwa taasisi nyingine kujitokeza kusaidia mashindano hayo ya ili kuweza kuwafikisha
mbali wanamichezo hao wenye uwezo mkubwa wa kufanya mchezo huo kufikia hata
kiwango cha Kimataifa.
Kwa upande wa
Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Baiskeli Bw.Godfrey Mhagama alisema kwa mwaka
huu kuna zaidi ya wachezaji 200 waliyoshiriki mshindano haya ombi langu kwa serikali ifatafute wadau watakao weza kusaidia
kuendeleza vipaji vya vijana hawa kanda ya ziwa iliwaweze kuufanya mchezo
huu kuwa ajira na kupata mafanikiwa makubwa kama wachezaji wa ulaya.
“Wakazi wa Kanda ya Ziwa
wa wanauwezo mkubwa katika uendeshaji wa
baiskeli hii ni kutokana na utamaduni
wao wa kutumia Baiskeli kama chombo cha usafiri”,alisema Bw.Mhagama.
Naye Meneja wa Mgodi
wa Acacia Buzwagi Bw.Asa Mwaipopo alisema
katika mashindano hayo ya mwaka huu watatoa zawadi kuanzia mtu wa kwanza mpaka
wa 30 na katika mashindano hayo wanaume watakimbia kilomita 156 na wanawake
kilomita 80 na zawadi ya mshindi kwanza
kwa mwanaume ni milioni moja na nusu na kwa wanawake ni
milioni moja.
Pamoja na hayo wanamichezo
hao wameaswa kufanya juhudi katika mchezo huu pia kutojaribu kutumia madawa ya
kuongeza nguvu wakati wa michezo.
*******************MWISHO********************
0 comments:
Post a Comment