Home » » Wanahabari watembelea machimbo ya alimasi Kongwa.

Wanahabari watembelea machimbo ya alimasi Kongwa.


Na Mwandishi Wetu, Songwa-Shinyanga
Baadhi ya waandishi kutoka jijini Dar es Salaam na mkoani Shinyanga wametembelea machimbo ya almasi yanayofanywa na wananchi eneo la mjini mdogo wa Songwa.
Ziara ya waandishi hao imekwenda sambamba na kufanya uchunguzi juu ya huduma mbalimbali za kijamii zinazotolewa na Serikali kwa wakazi wa maeneo hayo, yaliomo ndani ya Wilaya ya Kishapu Mkoa wa Shinyanga.
Waandishi hao wameshuhudia namna wananchi na hasa vijana wanavyojishughulisha na shughuli nzima za machimbo ya madini ya almasi licha ya Kata ya Songwe kukabiliwa na huduma duni za maji safi na salama kwa matumizi yao pamoja na yale ya shughuli za machimbo.
Mtandao huu utawaletea mahojiano ya wananchi eneo hilo pamoja na hali halisi ya huduma anuai za kijamii kwa wakazi wa Kata hiyo ya Songwa iliyopo Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga muda si mrefu.
Chanzo: Mo blog

0 comments:

 
Supported by Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa