Home » » Bob Makani kuzikwa leo Shinyanga

Bob Makani kuzikwa leo Shinyanga


Mwandishi wetu, Shinyanga Yetu
MWILI wa Mwasisi wa Chadema, Ali Makani au maarufu kwa jina la Bob Makani (76) ambaye alifariki dunia mwishoni mwa wiki unazikwa leo katika Kijiji cha Negesi, Wilaya ya Kishapu, Shinyanga.
Bob Makani ambaye alikuwa akiugua kwa muda mrefu, alifariki Juni 9 mwaka hu majira ya saa 4.15 usiku katika Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam alikopelekwa baada ya kuzidiwa ghafla.

Hapo jana maelfu ya wakazi wa Manispaa ya Shinyanga na makada wa Chadema, walijitokeza kwa wingi kwenye viwanja vya Shycom mjini hapa kutoa heshima zao za mwisho kwa muasisi wa chama hicho, Mohamed Bob Makani.
Chadema kilisema watamuenzi muasisi huyo kwa kuendeleza mapambano Bungeni, hususan katika Bunge la Bajeti ambalo limeanza jana.

Akizungumza mkoani hapa, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, John Mnyika, alisema wabunge wa chama hicho watamuenzi Bungeni kwa vitendo kwa kusimamia masuala aliyoyapa kipaumbele.

Mnyika alisema wataanza kumuenzi Makani katika mkutano wa Bunge unaoendelea kwa niaba ya wananchi wa Shinyanga na Watanzania kwa kusimamia haki, uwajibikaji na mabadiliko kwenye mfumo wa utawala, mambo ambayo  alikuwa akisisitiza wakati wa uhai wake.

“Wakati wa uhai wake Mzee Makani alikuwa akisema anawapenda Watanzania kila mara, hivyo tuendelee kumuombea kama ambavyo alitupenda ili jina lake liendelee kudumu siku zote,” alisema.
Mnyika alisema hayo baada ya wananchi kupaza sauti ya kutaka apewe nafasi ya kuzungumza wakati wa kutoa heshima ya mwisho kwa mwili wa marehemu.

0 comments:

 
Supported by Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Shinyanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa