Mwandishi wetu, Kahama
ZAIDI ya wanafunzi Laki Mbili katika mikoa mitatu ya Dodoma,Morogoro na Shinyanga watanufaika na mradi wa Sauti yangu Haki yangu uliozinduliwa wilayani Kahama na kupokelewa na wadau mbalimbali wa elimu.
Msimamizi wa Mradi huo Gerald Ng’ong’a amesema mradi huo ni wa miaka mitatu ambao utazilenga Halmashauri zote za mikoa hiyo na wilayani Kahama umeanza kwa shule Kumi na Tatu,ukiwa na lengo la kuwajengea uwezo wanafunzi kutumia mabaraza ya kidemokrasia katika kutatua matatizo yao.
Ng’ong’a amesema mradi huo pia mbali ya kuwajengea uwezo wanafunzi pia utawashirikisha walimu zaidi ya elfu Mbili,wazazi na maafisa katika Halmashauri za mikoa hiyo hatua itakayosaidia kuboresha demokrasia ya kuchagua na kuchaguliwa sambamba na kupanua wigo wa elimu.
Katibu Tawala wa wilaya ya Kahama bwana Ernest Masanja amesema Serikali itahakikisha inaupokea mradi huo na kusimamia ipasavyo ili utakapomaliza muda wake jamii ipate uelewa wa kuondoka ulipoishia na kwenda hatua nyingine.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment