Mwandishi wetu, Kahama
MBUNGE wa Jimbo la Kahama, James Lembeli amekataa taarifa ya serikali ya kijiji cha Chambo kwa madai iliandaliwa na viongozi bila kuwashirikisha wananchi.
Katika mkutano wake uliofanyika katika kijiji hicho Lembeli alidai taarifa hiyo haiendani na mahitaji ya wananchi hivyo aliwataka viongozi hao kuacha tabia ya kujifungia ofisini na kuandaa taarifa bila kuwashirikisha wananchi wenyewe.
Kukataa kwa taarifa hiyo kulikuja baada ya wananchi kulalamikia tatizo la ukame wa maji na upungufu wa Chakula katika kata hiyo ya Chambo huku taarifa ya serikali ya kijiji hicho haikufafanua matatizo hayo.
Aidha Lembeli aliwataka wananchi wenyewe waeleze matatizo yao ndipo walipodai hali ngumu ya upatikanaji wa chakula na maji hali ambayo mbunge huyo aliwachangia shilingi 1,300,000/= na kuwataka viongozi hao wasimamie matumizi yake kwa mujibu wa mahitaji ya kijiji hicho.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment