Mwandishi wetu, Kahama-Shinyanga Yetu
HALMASHAURI za wilaya, miji, Manispaa na Majiji
zimetakiwa kutenga bajeti ya kusaidia shule binafsi kwa kuwa mchango zinazotoa
katika Taifa ni sawa na zile za Serikali ambazo zinapata misaada mingi kutoka
serikalini.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya
Mhongolo iliyopo wilayani Kahama Jeremiah Gunda wakati akitoa taarifa fupi
kwenye mahafari ya saba ya Shule hiyo.
Katika mahafari hayo Mwalimu gunda alisema shule hizo
binafsi zinazalisha watoto wengi kwenda kupata elimu za juu lakini Serikali
haizishirikishi ikiwemo walimu wake kuwapeleka kwenye semina mbalimbali
zitolewazo kupitia Halmashauri hizo.
Hata hivyo Afisa Elimu Taaluma katika Halmashauri ya mji wa
Kahama;bi Annastazia Manumbu alisema hali hiyo inawezekana kwakuwa mchango
mkubwa utolewao na shule hizo kitaaluma huonekana katika jamii hivyo alisema
atalifikisha kwenye vikao husika .
Manumbu amewataka wazazi wasibweteke na elimu waliyoipata
watoto wao hivyo wakati wa kusubiri matokeo ya mitihani yao ni bora
wakawapeleka kujiendeleza na masomo mengine kuliko kuwaacha wakizagaa mitaani
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment