Mwandishi wetu, Kahama-Shinyanga Yetu
ZAIDI ya bodaboda mia saba wanaofanya biashara ya
kusafirisha abiria kwa kutumia pikipiki wilayani Kahama wamepatiwa mafunzo ya
usalama barabarani hali itakayopunguza vifo vitokanavyo na ajali.
Mkuu wa Usalama barabarani wilayani Kahama Mkaguzi Msaidizi
bwana Robert Siwendo amesema mafunzo hayo yamedhaminiwa na benki ya CRDB Tawi
la Kahama na kuwashirikisha vijana hao wa Bodaboda.
Aidha bwana Siwendo amesema mafunzo hayo yamekuja baada ya
idadi kubwa ya vijana hao kubainika wanafanya shughul hizo bila kufuata misingi
ya Sheria ya usalama barabarani ikiwemo kuendesha pikipiki bila kuvaaa kofia
nzito pamoja na wengine kutokuwa na reseni.
Amesema mbali na hayo pia pikipiki hizo zimekuwa zikikodiwa
na Waharifu hali ambayo imekuwa ikihatarisha maisha yao kwa kuuawa na
kunyang’anywa mali zao ikiwa sababu kubwa ni vijana hao kutokuwa makini wakati
wa kazi zao.
Kwa upande wake Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Kahama
iliyodhamini mafunzo hayo bwana Said Pamuye amesema utaratibu huu utakuwa
endelevu kwani kuwapa mafunzo hayo watakuwa na uwezo wa kufahamu sheria za
Usalama barabarani hali itakayopunguza matatizo wanayokumbana nayo wakiwa
kazini.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment